Dodoma/Dar.
Waziri wa Fedha, Saada Mkuya leo atawasilisha bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha wa 2015/16 ambayo wachambuzi wameielezea kuwa itakuwa na unafuu kwa wananchi kutokana na Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba, mwaka huu.
Waziri wa Fedha, Saada Mkuya leo atawasilisha bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha wa 2015/16 ambayo wachambuzi wameielezea kuwa itakuwa na unafuu kwa wananchi kutokana na Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba, mwaka huu.
Wakati wachambuzi wakiielezea kuwa ni bajeti ya uchaguzi, wabunge waliozungumza na Mwananchi jana walisema hawatarajii kitu kipya kwa kuwa kila mara wamekuwa wakiipitisha kwa makofi, lakini utekelezaji unakuwa mdogo na sababu zimekuwa ni ukosefu wa fedha.
Bajeti hiyo ya Sh22.4 trilioni, ongezeko la
asilimia 16 kulinganisha na bajeti ya mwaka 2014/15 ya Sh19.6 trilioni,
inatarajiwa kuboreshwa kwenye maeneo kadhaa baada ya wabunge kuchachamaa
wakati wa uwasilishaji wa bajeti za wizara mbalimbali.
Wabunge waligeuka mbogo wakati wa upitishaji wa bajeti za wizara hasa kutokana na Serikali kushindwa kupeleka fedha za miradi ya maendeleo kwa angalau asilimia 50 ya fedha zilizotengwa kwenye bajeti inayomalizika, na wakati mwingine ilibidi Waziri Mkuya asimame kutoa ahadi kuwa masuala hayo yangepelekwa kwenye Kamati ya Bajeti kuboreshwa.
Hii ni mara ya pili kwa Waziri Mkuya kuwasilisha
bajeti baada ya kufanya hivyo kwa mara ya kwanza mwaka jana
alipowasilisha ya mwaka unaomalizika Juni 30.
Akiwasilisha taarifa ya mwelekeo wa bajeti kwa
mwaka wa fedha 2015/16 unaoanza Julai Mosi, Mkuya alisema Serikali
imepania kupunguza utegemezi wa fedha kutoka kwa wahisani na wafadhili
kutoka asilimia 14.8 hadi asilimia 8.4 na kwamba itajikita zaidi katika
kukusanya kodi kwa kuhimiza matumizi ya vifaa vya kielektroniki.
Wachambuzi walihojiwa na Mwananchi jana walielezea bajeti hiyo kuwa italenga zaidi kutoa matumaini kwa wananchi, lakini itakuwa vigumu kutekelezeka.
“Kwa mfano, kupunguza utegemezi kwa wahisani ni
tumaini zuri, lakini shaka ni malimbikizo ya madeni kwa makandarasi,
walimu na taasisi nyingine zinazojiendesha. Tatizo jingine ni bajeti
kidogo iliyotengwa kwa maendeleo,” alisema Profesa Humphrey Moshi kutoka
Idara ya Uchumi ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).
Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Ezekiah Oluoch alisema bajeti hiyo haina matumaini kwa watumishi wa umma hususani walimu nchini kutokana na mambo mengi kutoonekana.
“Niliangalia kwa umakini bajeti ya elimu na
kuichambua, lakini mambo mengi ya msingi hayajaonekana. Mfano fungu la
kulipa madeni ya walimu wastani wa Sh20 bilioni halipo, bajeti ya
kuanzisha Tume ya Utumishi wa Walimu hakuna.”
Mbali na kupunguza utegemezi kwa nchi wahisani na
wafadhili, Serikali pia ilitangaza nafuu kubwa katika ada na kodi
mbalimbali za ardhi, baada ya kuzishusha kwa wastani wa asilimia 50,
jambo linaloonekana kuwa la kuwapa matumaini wananchi wakati huu wa
kuelekea Uchaguzi Mkuu.
Katika taarifa ya mwelekeo wa bajeti kwa mwaka wa
fedha 2015/16 unaoanza Julai Mosi, Mkuya alitangaza vipaumbele vyake,
ikiwamo kugharamia uchaguzi mkuu, kukamilisha miradi inayoendelea,
kuweka msukumo maalumu kwenye miradi ya umeme vijijini, maji vijijini na
kuimarisha rasilimali watu.
Mkuya alisema sura ya bajeti inaonyesha kuwa Sh22,480.4 bilioni zinatarajiwa kukusanywa na kutumika katika mwaka ujao wa fedha.
Changamoto za 2014
Mkuya alisema katika kukabiliana na changamoto hizo, Serikali itaboresha na kuimarisha mifumo ya ukusanyaji na usimamizi wa mapato, kuendelea kusisitiza matumizi kulipa kodi na tozo kwa kutumia EFD’s, kuhakikisha hakuna kuingia mikataba mipya ya miradi na huduma bila kuwa na uthibitisho wa kuwapo fedha; kuboresha mazingira ya uwekezaji kwa lengo la kuvutia uwekezaji wa ubia kati ya sekta binafsi na sekta ya umma.
Waziri Mkuya alisema Serikali itaendelea na juhudi za kuimarisha
ukusanyaji wa mapato ya ndani kwa kuchukua hatua mbalimbali za kisera
na kiutawala kwa lengo la kuongeza mapato kwa kuimarisha usimamizi wa
vyanzo vya mapato.
Waziri wa Fedha alisisitiza matumizi ya vifaa na
mifumo ya kielektroniki katika ukusanyaji wa kodi ili kuongeza ufanisi
katika ukusanyaji na kudhibiti wa mapato.
Alisema anakusudia kuhakikisha kuwa taasisi,
wakala, mamlaka zinazojitegemea na mashirika ya umma yanakusanya
ipasavyo mapato yasiyo ya kodi ili kupunguza utegemezi kutoka Serikali
kuu.
Pia atapitia upya baadhi ya viwango vya kodi, ada na tozo mbalimbali ili viendane na hali halisi ya utoaji wa huduma husika.
Mkuya alisema sura ya bajeti inaonyesha kuwa Sh22,480.4 bilioni zinatarajiwa kukusanywa na kutumika katika mwaka ujao wa fedha.
Jumla ya mapato ya ndani yanatarajiwa kuwa Sh14,824.4 bilioni, sawa na asilimia 57.8 ya bajeti yote.
Alisema washirika wa maendeleo wanatarajiwa
kuchangia Sh1,888.2 bilioni sawa na asilimia 8.4 ya bajeti
ikilinganishwa na asilimia 14.8 ya bajeti ya mwaka 2014/2015 ambazo
sehemu kubwa ni mikopo
ya masharti nafuu.
ya masharti nafuu.
Baadhi ya mikakati ya Serikali katika mwaka huo wa
fedha ni kuendelea kudhibiti kasi ya mfumuko wa bei na kuhakikisha kuwa
unabaki kwenye wigo wa tarakimu moja, kuongeza ukusanyaji wa mapato ya
ndani ikijumuisha mapato ya halmashauri kufikia asilimia 15.7 ya Pato la
Taifa pamoja na kuongeza mapato yatokanayo na kodi kufikia asilimia
14.2 ya Pato la Taifa.
Changamoto za 2014
Waziri Mkuya alizitaja changamoto za bajeti ya
mwaka 2014/2015 kuwa ni kutokufikia malengo ya kukusanya mapato ya kodi
na yasiyo ya kodi; Wafanyabiashara kugomea matumizi ya mashine za
kielektroniki za ulipaji kodi (EFD’s) na mapato ya ndani na nje
kutokupatikana kama ilivyokadiriwa.
Bajeti pia iliathiriwa na sera kulazimika kutoa
fedha kwa mashirika ya umma ya biashara kama vile ATCL, TRL na Tazara,
mahitaji makubwa ya kuboresha miundombinu ya maji, reli, bandari,
viwanja vya ndege na barabara ili kukuza uchumi na kuongeza ajira na
mchakato mrefu wa kupata mikopo ya kibiashara.
Mkuya alisema katika kukabiliana na changamoto hizo, Serikali itaboresha na kuimarisha mifumo ya ukusanyaji na usimamizi wa mapato, kuendelea kusisitiza matumizi kulipa kodi na tozo kwa kutumia EFD’s, kuhakikisha hakuna kuingia mikataba mipya ya miradi na huduma bila kuwa na uthibitisho wa kuwapo fedha; kuboresha mazingira ya uwekezaji kwa lengo la kuvutia uwekezaji wa ubia kati ya sekta binafsi na sekta ya umma.
Wasiwasi wa wabunge
Wakizungumza katika mahojiano na Mwananchi jana,
baadhi ya wabunge walionyesha wasiwasi kuhusu utekelezaji wa bajeti
tajwa kwa kuwa tatizo lililopo ni upatikanaji wa fedha.
Walisema wanaandaa bajeti nzuri, iliyokamilika,
lakini utekelezaji wake unakuwa wa nadharia, haitekelezeki na
ikitekelezeka inakuwa asilimia 30.
Ezekiel Maige, Msalala (CCM), alisema kuwa
ukisiaji wa mapato na nidhamu ndogo ya matumizi ndio tatizo kubwa.
“Tunakadiria mapato na matumizi wakati hatuna fedha na matokeo yake
fedha hazipatikani tunashindwa kufikia malengo.
“Vilevile, hata fedha zinazopatikana, nidhamu ya
matumizi haipo, watu ‘wanapiga hela’ ukiangalia ripoti ya CAG unaweza
kulia, uanzishwaji wa miradi isiyokuwa ya mipango na kutumia fedha kama;
vitambulisho vya taifa, uandikishaji wa BVR, wanatumia mabilioni ya
shilingi wakati hazikuwa katika mafungu. Kashfa zimejaa za ubadhirifu
lakini iliyoonekana tu ni ya Richmond,” alisema Maige.
Mariam Msabaha (viti maalumu, Chadema) alisema,
“Hapa ni yaleyale ya kila mwaka, tunajaribu kupitisha bajeti kwa kupiga
makofi, lakini hakuna kinachofanyika na ukiuliza unaambiwa fedha hakuna
na kama zipo utekelezaji wake ni chini ya asilimia 30.
Mbunge wa Gando (CUF), Khalifa Suleyman Khalifa
alisema bajeti kuongezeka ni ishara njema kuwa sasa fedha zitapatikana
zaidi na zitaelekezwa katika maeneo muhimu ya afya, elimu na kilimo.
“Tatizo hapa ni fedha, sasa Serikali ikitaka
heshima, kile ambacho Bunge linapanga, fedha zipelekwe kama
inavyohitajika na inavyokusudiwa,” alisema.
Kwa upande wake, Augustino Mrema (Vunjo-TLP),
alisema imekuwa ni kawaida kuimba masuala ya bajeti lakini hakuna
utekelezaji wa miradi.
“Hakuna cha kusema kuwa bajeti itakuwa na kipya
kwa kuwa kila mwaka tunapanga bajeti lakini fedha haziendi kwenye miradi
na zaidi ya hapo ni chini ya makadirio,” alisema Mrema.
Mbunge wa viti maalumu (CCM), Esther Bulaya
alisema: “Hakuna kipya kama tunategemea fedha za wahisani, huwezi kuweka
mipango kwa fedha ambayo hujui utaipataje na utaipata lini.”
Mbunge mwingine, Zarina Madabida (viti maalumu-
CCM), alisema: “Tatizo Serikali inaangalia fedha za wahisani ambazo
hazina uhakika. Kinachotakiwa ni Serikali kuongeza nguvu katika
makusanyo yake ya vyanzo ambayo ndiyo vya uhakika zaidi.
“Ni muhimu Serikali kusimamia mapato yake yatokanayo na kodi, wanaokwepa kodi wabanwe, na idhibiti ukusanyaji,” alisema.
Salum Barwani (Lindi Mjini-CUF) alisema, “Kipindi
chote cha bajeti ni funika kombe mwanaharamu apite. Bajeti ni tendo la
kisheria, inatakiwa Bunge liambiwe mwaka jana kilifanyika nini na mwaka
huu kuna nini. Mwaka jana tatizo lilikuwa nini na mwaka huu tufanye nini
tusirudie njia ileile, kimsingi, hatutarajii mapya,” alisema.
Mbunge wa Kawe, Halima Mdee (Chadema)
alisema,“Siamini kama kutakuwa na mabadiliko chanya. Kila mwaka
tunatengeneza bajeti nzuri, tunaipigia makofi tukiamini sasa miradi
inatekelezwa, lakini hakuna kinachofanyika.
“Sitarajii mabadiliko na ukiuliza unaambiwa tatizo
ni upatikanaji wa fedha, ninadhani kitakachofanyika ni kucheza na
tarakimu tu.”
William Ngeleja (Sengerema-CCM) alisema:
“Matarajio si mapya, tunaamini mambo yatakuwa mazuri ikiwa Serikali
itasikiliza ushauri wa Bunge.”
Katika hatua nyingine, wachambuzi wa masuala ya
kiuchumi wameitaka Serikali kuepuka utamaduni wa kutapanya fedha katika
mgawanyo wa bajeti badala yake iwekeze fedha nyingi katika sekta chache
na nyeti.
Mwenyekiti wa Shirikisho la Wenye Viwanda nchini
Tanzania (CTI), Felix Mosha alitaja mambo manne yanayotakiwa kupewa
kipaumbele ili kuongeza kasi ya maendeleo nchini.
Mambo hayo ni kilimo, reli, elimu na viwanda
ambayo yanapaswa kutengewa angalau asilimia 50 ya bajeti yote ili
kupunguza changamoto zilizopo katika maeneo hayo.
“Tumekuwa na sera ya kilimo kwanza lakini Rais
Jakaya Kikwete amekiri kuwapo changamoto katika utekelezaji wake,
tulishindwa hata kufikia makubaliano ya mkataba wa Maputo, uliozitaka
nchi za Afrika angalau kutenga asilimia 10 ya bajeti yake wakati
tunatambua kilimo ndiyo muhimili wa uchumi wa Taifa,” alisema.
“Ukiangalia elimu, viwanda na njia za reli ni
maeneo nyeti, lakini hakuna dhamira ya uwekezaji wa kutosha. Ningetamani
kuona angalau asilimia 50 ikitengwa kwa ajili ya maeneo hayo tu kuliko
kugawa kidogo kidogo, hatuwezi kufika.”
CHANZO: MWANANCHI
CHANZO: MWANANCHI
No comments:
Post a Comment