Wakala
wa mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania Mbwana Samatta, Jamal Kisongo
amesema hatma ya mshambuliaji huyo kucheza soka la kulipwa Ulaya sasa
itasubiri mwakani kutokana na rais na mmiliki wa klabu yake yake TP
Mazembe Moise Katumbi kuonesha bado anahitaji huduma yamchezaji huyo
hususan katika michuano ya vilabu bingwa barani Afrika.
“Katumbi ameonesha bado anahitaji
kumtumia katika kikosi chake kwenye michuano ya champions league kwa
maana hiyo makusudio yetu na matarajio yetu, kunatimu moja kubwa ilitaka
kumsaini kwa ‘Euro’ milioni moja lakini bahati mbaya Katumbi alitaka
amuache baada ya champions league kuisha”, amesema wakala huyo wa
Samatta.
“Kwahiyo hili tulilitazama kwa
upande wetu na kuona si jambo la busara kama ni biashara hiyo ni bora
abaki tu mpaka Januari ili aweze kuondoka kama mchezaji huru na yeye
kuweza kufaidika zaidi kama mchezaji na si kuinufaisha TP Mazembe”,
amesema.
“Kwa kawaida, huwa sio vizuri
sana kuviweka hivi vitu wazi, kwasababu ni mapema, lakini kwa hiyo timu
waliokuwa wanataka kutoa kiasi hicho cha pesa ilikuwa siyo klabu ya
Ulaya, ilikuwa ni klabu moja kubwa ya Afrika. Na hicho ndio kitu
kimojawapo kilichochangia kukataa ofa hiyo, kwasababu kusudio letu kubwa
lilikuwa ni kuhakikisha kwamba Samatta anacheza mpira Europe”,
amefafanua.
“Sisi tunataka hata kama pesa
itakuwa ndogo lakini aende akacheze soka Ulaya na kufungua milango kwa
wenzake hata kama pesa ni ndogo. Tunauhakika kama ataweza kucheza Ulaya
kwa mwaka mmoja, basi anauwezo wa kutengeneza pesa nyingi na timu kubwa
zitakuwa zimeshaingia kwenye vita kubwa ya kumsaka”, ameeleza.
“Tumeshapokea ofa nyingi zaidi ya
sita timu hasa zinamuhitaji, anahitajika na timu nyingi. Tumepokea ofa
kutoka Uswis, Ufaransa, Hispania na maeneo mengine. Ni mchezaji ambaye
yupo kwenye soko la Ulaya na timu zinamuhitaji”, alimaliza.
No comments:
Post a Comment