SIKU zikiwa zinahesabika kufikia Agosti 22, ndani ya Ukumbi wa Makumbusho, Posta jijini Dar ambapo shindano la kusaka vipaji vya kuigiza la Tanzania Movie Talents (TMT) linatarajiwa kufika kileleni, mshindi katika shindano hilo anatarajiwa kuweka historia ya aina yake.
Akizungumza na Centre Spread, Meneja Mradi wa TMT, Saul Mpock alisema kuwa mwaka jana ambao ulikuwa ni msimu wa kwanza wa shindano hilo, Mwanaafa Mwinzago (13) alikuwa mshindi na kuweka rekodi ya mtoto mdogo kushinda shindano hilo kubwa lililoshirikisha vijana kwa wazee na kujinyakulia kitita cha shilingi milioni 50.
“Msimu huu wa pili mambo yamekuwa tofauti kutokana na washiriki wote kuwa vijana na hakuna mtoto hata mmoja, hivyo basi mshindi anatarajiwa kuwa kijana na kuweka rekodi mpya,” alisema Mpock.
No comments:
Post a Comment