Wadaiwa
16 waliokwepa kulipa kodi ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), baada ya
kutorosha kontena za mizigo yao kwenye Bandari Kavu (ICD) ya Azam
mwishoni mwa mwaka jana, mali zao zinaanza kukamatwa leo na kufilisiwa.
Mkurugenzi
wa Mtendaji wa Kampuni ya Udalali ya Yono, iliyopewa kazi ya kufuatilia
wadaiwa hao wakiwemo baadhi ambao wamekamilisha malipo, Yono Kevella
alisema hayo Dar es Salaam jana.
Kevela
alisema kuanzia leo wanakaa na vyombo vya dola, kuanza utaratibu wa
kukamata na kufilisi mali za wahusika na kuwafikisha kwenye vyombo vya
sheria.
Kevela
alisema hadi sasa hakuna zuio lililotolewa, linazowazuia kutekeleza
wajibu wao katika kukusanya madeni hayo. Hata hivyo alisema, wengi wa
wadaiwa baada ya kutolewa kwa muda huo wa siku 14, wameonesha moyo wa
kulipa.
Wadaiwa 16 hawajamaliza madeni
Alitaja
wadaiwa 16 ambao hawajalipa madeni yao wala kupunguza, ambao
watafilisiwa wasipojitokeza kufanya malipo ni Said Ahmed Said Sh
28,249,352.50, Strauss International (45,393,769.95), Farid Abdallah
Salum (52,185, 614.97).
Wengine
ni Nasir Saleh Mazrui (60,105,873.77), Simbo Yona Kimaro
(64,221,009.10), Ally Masoud Dama (102,586,719.22) na Juma Kassem Abdul
(130,182,395.12), Salum Link Tyres (233,447,913.31) na Tybat Trading
Co.Ltd (448,690,271.90).
Pia
wamo IPS Roofing Co.Ltd (966,723,692.10), Tuff Tyres General Co Ltd,
(7,435,254,537.03), Swalehe Mohamed Swalehe (34,687,165.00), Rushwheel
Tyre General Co Ltd, (1,802,988,679.20), Said Ahmad Hamdan
(68,362,558.31), Ahmed Saleh Tawred ( 59,237,578.40) na Farida Abdullah
Salem Sh 75,334,871. 85.
Akizungumzia
wadaiwa waliolipa ndani ya siku 14 walizopewa na zikaisha juzi, alisema
wanane kati ya 24, ndiyo walijitokeza kulipa madeni baada ya kampuni
yake kuwafuatilia.