EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Saturday, March 2, 2013

Kiongozi mmoja mkuu wa Al Qaeeda auawa

Kiongozi mmoja mkuu wa kundi la wapiganaji la al-Qaeda ameuawa nchini Mali. Taarifa hizi zimethibitishwa na Rais wa Chad, Idriss Deby
 
Alisema kuwa majeshi ya nchi yalimuua Abdelhamid Abou Zeid, wakati wa makabiliano yaliyotokea katika eneo moja la vijijini nchini Mali.

Anasemekana kuwa wa pili kwa ngazi ya uongizi katika kundi hilo ambalo linapigana na majeshi ya kigeni nchini Mali.
Raia huo wa Algeria anatuhumiwa kwa mauaji ya mateka wawili kutoka nchi za magharibi Edwin Dyer raia muingereza mwaka 2009 Michel Germaneau raia wa ufaransa mwaka uliofuata.

Chadema yamng’ang’ania Kawambwa

WAKATI Waziri Mkuu, Mizengo Pinda ameunda tume kuchunguza matokeo mabaya ya mtihani wa Kidato cha Nne mwaka 2012, Chadema kimesisitiza msimamo wake kwamba kitafanya maandamano kushinikiza Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa na Naibu wake, Philipo Mulugo wajiuzulu.
 
Mapema wiki iliyopita Pinda alitangaza kuunda tume kuchunguza matokeo hayo, hatua ambayo Rais Jakaya Kikwete alitangaza kuiunga mkono katika hotuba yake ya mwisho wa mwezi aliyoitoa juzi.

Lakini jana Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alisema watafanya maandamano makubwa aliyoyaita ya kihistoria, katika mikoa ya Mwanza, Arusha, Mbeya na Dar es Salaam ili kushinikiza kutekelezwa kwa hatua hiyo.

Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara katika Viwanja vya Shule ya Sekondari Mtatatila, Sumbawanga mkoani Rukwa, Mbowe alisema: “Lengo la maandamano ni kuwataka waziri wa elimu na naibu wake wajiuzulu kwani wameshindwa kutekeleza majukumu yao ipasavyo na kusababisha watoto wa maskini kufanya vibaya kwenye mitihani yao.”

Je, kujamiiana huondoa msongo wa mawazo kwa wanawake?

UTAFITI uliofanywa na Chuo Kikuu cha State cha jijini New York nchini Marekani unaeleza kuwa manii ni nzuri kwa wanawake kwani huwaondolea msongo wa mawazo.
 
Pia, watafiti hao wamesema wanawake wanaofanya tendo la ndoa mara kwa mara bila kutumia kinga (mapenzi salama) wanakuwa na kiwango kidogo cha msongo wa mawazo na hufanya vizuri katika vipimo vya akili.

Hali hii wamesema wataalam hao kuwa inatokana na manii kuwa na kemikali ambazo humfanya mtu kuwa vizuri kihisia, huongeza upendo/unyenyekevu, huchochea mtu kupata usingizi na huwa na angalau aina tatu za kemikali za kuondoa msongo wa mawazo (anti-depressants).

Serikali yaanza kujenga kiwanda gesi Mtwara

HATIMAYE ujenzi wa kiwanda cha kusafisha gesi kabla ya kusafirishwa kwenda Dar es Salaam umeanza mkoani Mtwara.
 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi alisema jana kuwa ujenzi huo unaofanywa na Kampuni ya China Petroleum and Technology Development Co-operation (CPTDC), ambao awali, ulipaswa kuanza wiki iliyopita, umeanza juzi baada ya Serikali kufikia mwafaka na wananchi wa Kijiji cha Msimbati kinapojengwa.

“Mkuu wa Wilaya ya Mtwara (Wilman Ndile) na vijana wake walilazimika kufika Kijiji cha Msimbati, ambako wananchi walikuwa na mgogoro na watu wa Marine Park,” alisema Maswi.

Alisema baada ya ziara hiyo kushindwa kufanyika Jumapili iliyopita, uongozi wa wilaya ulikutana na viongozi wa kijiji na kufikia mwafaka uliofanikisha kuanza kwa ujenzi huo.
Alisema kuanzia mradi huo kutatoa ajira za kawaida kwa wakazi saba wa maeneo yanayozunguka mradi huo na kwamba kazi hiyo itaongeza mahitaji ya bidhaa mbalimbali na huduma katika Kata ya Msimbati
“Mathalan kuku, matunda na mboga za majani vinahitajika sana. Sasa wananchi ambao awali, hawakutaka kuelezwa lolote, wameanza kuchangamkia fursa hizo jambo ambalo litawanufaisha zaidi,” alisema.

Friday, March 1, 2013

Rufaa ya @JohnMnyika dhidi ya Uendeshaji wa Bunge wa Job Ndugai

RUFAA DHIDI YA UENDESHAJI WA BUNGE USIOKUWA WA HAKI NA UKIUKAJI WA KANUNI WA NAIBU SPIKA JOB NDUGAI KATIKA KUONDOA HOJA BINAFSI YA MAJI
Tarehe 28 Februari 2013 nimewasilisha rasmi rufaa kwa mujibu wa Kanuni ya 5 (4) dhidi ya uendeshaji wa Bunge usiokuwa wa haki wa Naibu Spika Job Ndugai kwa kukiuka kanuni ya 58 (5) kwa kulihoji bunge kinyume na kanuni kufanya uamuzi badili wa kuondoa hoja binafsi kuhusu hatua za haraka za kuboresha upatikanaji wa majisafi na ushughulikiaji wa majitaka katika Jiji la Dar es salaam.

Nimefanya hivyo baada ya kupata kumbukumbu rasmi ya Bunge (Hansard) za kikao cha tano cha tarehe 4 Februari 2013 cha mkutano wa kumi wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Katika Mkutano huo Naibu Spika Job Ndugai alisema na kufanya maamuzi kwamba: “Sasa ninahoji wanaoafiki kwamba hoja hii iondolewe waseme ndiyo…..hoja imeondolewa. Walioafiki Wameshinda”; wakati mtoa hoja sikuwa nimeomba idhini yoyote ya hoja yangu kuondolewa.

Jihadhari: Wanatapeli kwa kutumia maeneo na majina ya Ofisi za Serikali

Wimbo la utapeli limevamia kwa kasi ya ajabu katika mkoa  wa Iringa baada ya  wananchi kutapeliwa kupitia ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa, Theresia Mahongo na Mkuu  wa Mkoa  wa Iringa Dk Christine Ishengoma.

Matapeli hao  wamekuwa  wakiwapigia  watu mbalimbali simu na kuwataarifu kuwa katika  Ofisi hizo za viongozi wa Manispaa ya Iringa kuna pikipiki zimetolewa na Rais Jakaya  kikwete kwa ajili ya maofisa ugani na kuwa wao wamebahatika kuzipata mbili  hivyo wameamua kuziuza kwa bei ya Shilingi milioni 2.5 na kama mteja anahitaji afike ofisini hapo kulipa  pesa hiyo ili  apewe pikipiki na hati yake.

TUMA JINA LA MWANAMKE UNAYEDHANI ANAFAA KUTWAA TUZO YA 'WOMAN OF THE YEAR'

 
Chanzo cha hii habari ni www.globalpublishers.info soma zaidi

BETHIDEI YA LADNAA YAVUTIA MASTAA KIBAO


Jacqueline Wolper (kushoto), akimlisha keki Ladnaa kwenye Bethidei yake.
Ladnaa akiwa na keki yake.
Steve Nyerere akilishwa keki.

Wizi wa kutisha katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Dar es Salaam

IMEBAINIKA kuwapo kwa wizi wa kutisha katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Dar es Salaam, huku magari ya Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji yakitajwa kwamba yamekuwa yakivusha vifaa vya wizi kutoka ndani ya uwanja huo.
 
Wizi huo ambao umewasababishia hasara kubwa baadhi ya wasafiri wakiwamo wafanyabiashara, abiria wa kawaida na watalii wanaoingia nchini, unadaiwa kufanywa na baadhi ya wafanyakazi wa Wakala wa Mizigo wa Kampuni ya Swissport.

Wafanyakazi hao wamekuwa wakiiba vifaa na bidhaa kwa kuchana mabegi ya abiria kisha kuviweka kwenye makoti yao ya kazi lakini kwa mizigo mikubwa, wamekuwa wakiificha kwenye magari ya zimamoto ambayo huingia na kutoka ndani ya uwanja wa ndege bila kufanyiwa ukaguzi.

Chanzo kingine cha habari katika uwanja huo kinasema magari ya zimamoto yanayofanya kazi katika uwanja huo hayakaguliwi yanapopita kwenye lango kuu, hivyo kutoa mwanya wa kuvushwa kwa mali za wizi.

Adaiwa kumtoa mimba ‘baamedi’

POLISI Bunda wamesema watamfikisha mahakamani wakati wowote Ofisa tabibu mmoja wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda, anayetuhumiwa kumtoa mimba mhudumu mmoja wa baa ambaye kwa sasa hali yake ni mbaya.

Ofisa tabibu huyo Michael Musimu, ambaye amekuwa akifanya kazi katika kituo cha afya Manyamanya, kilichoko Bunda, anashikiliwa na polisi akituhumiwa kumtoa mimba  mhudumu mmoja wa baa ijulikanayo kwa jina la Savana, iliyoko mjini hapa.

Polisi wamemtaja mhudumu huyo kuwa ni Salome Saimon Bugunda, ambaye sasa hali yake ni mbaya na amepelekwa katika Hospitali ya Rufaa Bugando Mwanza kwa matibabu zaidi.

FBI watua Zenji kusaka wauaji wa Padri Mushi

ASKARI wa Shirika la Upelelezi la Marekani (FBI), wamewasili Zanzibar kufanya uchunguzi wa kuwabaini waliomuua kwa kumpiga risasi, Padri Evarist Mushi wa Kanisa Katoliki.
Kamishna wa Polisi wa Zanzibar, Mussa Ali Mussa alisema kwa simu jana kuwa wapelelezi wa kigeni wamewasili Zanzibar na tayari na wameanza kazi hiyo.
Wapelelezi hao wameingia kazini kushirikiana na wenzao wa Tanzania kuwasaka wauaji wa padri huyo aliyepigwa risasi Februari 17, mwaka huu.

Padri Mushi aliuawa asubuhi alipokuwa akienda kuongoza ibada katika Kanisa la Mtakatifu Teresia, Beit el Raas, nje kidogo ya Mji wa Zanzibar na kuzikwa Kitope, Kaskazini Unguja Februari 20, mwaka huu.

“Wapelelezi kutoka nje wamefika na wapo kazini,” Kamishna Mussa alisema bila ya kutaja wanatoka nchi gani.

Pia Kamishna Mussa hakutaka kueleza ni lini wapelelezi hao walifika Zanzibar na idadi yao kwa maelezo kwamba hizo ni siri za Polisi na zikivuja, zitaingilia uchunguzi wanaoufanya.
Hata hivyo, vyanzo vya ndani ya Serikali, vililithibitishia gazeti hili kuwa FBI walikuwa wameanza kuwasaka wauaji wa Padri Mushi.

CAG agundua madudu Tanesco

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh amesema uchunguzi alioufanya dhidi ya vigogo watatu wa Shirika la Ugavi wa Umeme (Tanesco), unaonyesha kuwa kuna madudu ya kutisha.
 
Utouh alisema hivi karibuni kuwa alijikita zaidi katika mikataba yenye thamani ya zaidi ya Sh500 milioni iliyoingiwa na shirika hilo.

Awali, Ofisi ya CAG ilitoa ripoti ambayo ilisababisha aliyekuwa Mkurugenzi wa Tanesco, William Mhando kusimamishwa na baadaye kufukuzwa.

Vigogo wengine waliotajwa katika ripoti hiyo, Robert Shemhilu, Ofisa Mkuu wa Fedha, Lusekelo Kassanga na Meneja Mwandamizi Ununuzi, Harun Mattambo walisimamishwa kazi ili kupisha uchunguzi wa tuhuma zinazowakabili ikiwa ni pamoja na kuingia mikataba mibovu wakati wa ununuzi wa mali za shirika.

MWANAMUZIKI NYOTA NIGERIA APIGWA RISASI ZA KICHWA NA KUFARIKI PAPO HAPO

MSANII Hip hop nchini Nigeria, Olaniyan Damilola maarufu kama Damino Damoche, jana mchana alipigwa risasi na kufariki papo hapo.
Damoche alipigwa risasi kwenye geti la la Chuo Kikuu cha Lagos State Ojo (LASU) alipokuwa akisomea Banking & Finance.
Msanii huyo alipigwa risasi mbili za kichwa na watu wanaohusishwa na imani kali za kidini muda mfupi baada ya kutoka kwenye mtihani.Damoche alijipatia umaarufu kwa wimbo wake “Obo to she”.

FERGUSON ASEMA NJIA NYEUPE KUTWAA MATAJI MATATU MSIMU HUU

Alex Ferguson
LONDON, ENGLAND
ALEX FERGUSON amewatia mzuka nyota wake akiwaambia kuwa wana nafasi ya kuweka majina yao katika vitabu vya historia kwa kutwaa mataji matatu kwa mpigo ‘treble’ msimu huu.
Bosi huyo wa Old Trafford anaamini kuwa United inaweza kurudia mafanikio ya mwaka 1999 waliposhinda mataji ya Premier League, FA Cup na Champions League.

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate