AWAMU YA PILI YA WANAFUNZI WALIOPANGIWA MIKOPO KWA 2015/2016
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) inapenda
kuwafahamisha waombaji wa mikopo kwa mwaka wa masomo 2015/2016 kuwa
imetoa Awamu ya Pili ya waombaji 28,554 waliofanikiwa kupata mikopo na
kufanya idadi ya waombaji wenye sifa wa mwaka wa kwanza waliofanikiwa
kupata mikopo hadi sasa kufikia 40,836.Katika awamu ya kwanza, Bodi ilitoa orodha yenye jumla ya waombaji 12,282 waliofanikiwa kupata mikopo.
Majina ya waombaji waliofanikiwa kupata mikopo kutoka katika awamu zote mbili yanapatikana kupitia mtandao wa Bodi wa olas.heslb.go.tz na tovuti ya Bodi (Bofya Hapa www.heslb.go.tz ) Aidha, orodha hizo pia zimetumwa vyuoni kwa ajili ya taratibu za usajili.
Lengo la Bodi ni kuhakikisha kuwa wanafunzi wa mwaka wa kwanza wenye sifa ya kupata mikopo katika mwaka wa masomo 2015/2016 wanapata mikopo na hivyo kupata elimu ya juu.
Aidha, Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu inapenda kuwasihi waombaji wa mikopo kuwa watulivu na kupuuza taarifa zinazosambaa katika baadhi ya mitandao ya kijamii kuwa Bodi haitatoa mikopo kwa waombaji kwa mwaka wa masomo 2015/2016.
Imetolewa na:
MKURUGENZI MTENDAJI
BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU
09 November 2015
No comments:
Post a Comment