EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Thursday, June 28, 2012

Madaktari waliomshambulia askari wajisalimishe - Kova

Wakati Dkt. Ulimboka alipofikishwa nje ya Kitengo cha Mifupa (MOI), Madaktari wenzake ambao wamesusa kuhudumia wagonjwa, walifurika hospitalini hapo na kuanza kusukuma gari hilo huku wakiimba nyimbo za mshikamano na wengine wakilia.

Hata hivyo, katika kile kilichoonekana ni kulipiza kisasi, Madaktari hao ghafla walimgeukia mmoja wa askari Polisi aliyekuwa amevalia kiraia na kumshambulia kwa kipigo kwa madai kuwa aliwasiliana na wenzake na kuwataarifu kuwa Dkt. Ulimboka bado yuko hai.

Askari huyo pia alinyang’anywa simu na redio ya mawasiliano ambavyo vyote viliharibiwa vibaya na  alionekana akiwa ameumizwa na kuvimba mwilini huku akiwa hajapatiwa huduma yoyote.

Kutokana na majeraha hayo, askari wenziwe walimuondoa eneo hilo; na mara moja Polisi katika Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, imewataka waliomshambulia askari huyo kujisalimisha. 
Kamanda wa Polisi wa Kanda hiyo, Suleiman Kova aliwataka Madaktari waliomshambulia askari huyo, wajisalimishe na kurudisha vifaa walivyomnyang’anya; simu na redio ya mawasiliano.

Kova aliyezungumza na waandishi wa habari kuhusu tukio hilo, alikemea tabia ya wananchi kujichukulia hatua mkononi kwa kumshambulia askari huyo na kuongeza kuwa alikuwa kazini akichunguza tukio hilo.

Mwenyekiti wa Chama cha Madaktari Tanzania (MAT), Dkt. Namala Mkopi, alidai Dkt. Ulimboka alitekwa juzi usiku na watu wasiojulikana na kupigwa na kung’olewa kucha na meno na hali yake ni mahututi.

Alidai Dkt. Ulimboka alizungumza kwa taabu alipofikishwa hospitalini ambapo alidai juzi jioni alipigiwa simu na mtu aliyejitambulisha kama Abduel anayedaiwa kutoka Ikulu na alitaka kuzungumza naye kuhusu maendeleo ya madai ya madaktari.

 “Alikubali kuonana na mtu huyo ambaye pia alikuwa akizungumza naye mara kwa mara na alikubaliana na wenzake asiende kuonana naye mwenyewe, aliongozana na rafiki yake Dk Deo hadi eneo walilopatana ambalo ni Kinondoni barabara ya Tunisia,” alisimulia Dkt. Mkopi. Alidai Dkt. Ulimboka alisimulia kuwa akiwa katika eneo hilo pamoja na Abduel na Dkt. Deo, walitokea watu watatu; wawili wakiwa na silaha aina ya bastola na mmoja bunduki.

Kwa mujibu wa madai ya Dkt. Ulimboka, watu hao walianzisha vurugu na kuwataka wengine waondoke na kumchukua peke yake na kumuingiza kwenye gari nyeusi yenye namba zisizosajiliwa na kutokomea naye.

Kwa mujibu wa madai hayo, Dkt. Deo aliamua kuwasiliana na wenzake ambao walimtafuta kwenye vituo vyote vya Polisi bila mafanikio na kuishia kuandika maelezo ya tukio hilo katika Kituo Kikuu cha Polisi.

Baada ya hapo, Dkt. Deo pia aliwasiliana na wanaharakati akiwamo Mkurugenzi wa Kituo cha Haki za Binadamu (LHRC) Hellen Kijo-Bisimba. Anadai alipokea simu kutoka kwa mtu aliyejitambulisha kuwa ni msamaria kwamba amemuokota Dk Ulimboka akiwa hoi eneo la Mabwepande.

Inadaiwa Dkt. Deo aliwachukua wanaharakati hao hadi Kituo cha Polisi Bunju alikopelekwa Dk Ulimboka na kumchukua na kumkimbiza Muhimbili.

Kova alisema Dkt. Ulimboka  alikuwa na rafiki yake aitwaye Dkt. Deogratius Michael na watu wengine katika Klabu ya Leaders Kinondoni ambapo ghafla saa 5:30 usiku, walitokea watu watano wasiofahamika wakavamia klabu hiyo na kuwatishia na kuwataka walale chini.

 “Dokta Ulimboka na wateja wengine walilala chini kwa kuhofia madhara kwa kuwa watu hao walikuwa na kitu wanachohisi ni silaha na hatimaye watu hao walimchukua Dkt. Ulimboka na kusema kwamba walikuwa wakimhitaji yeye na kumuingiza katika gari aina ya Suzuki Escudo nyeusi ambayo haikuwa na namba za usajili,” alidai Kova.

Alidai wakati wakiwa njiani, watu hao walianza kumshambulia sehemu mbalimbali za mwili wake na bila kusema wanataka nini kutoka kwake na walipofika maeneo ya Mwenge, walimvisha fulana nyeusi usoni na hakujua tena wanaelekea wapi huku wakiendelea kumpiga na mmoja wa watu hao akasema watamuua.

Kamanda Kova alidai ilipofika asubuhi, Dkt. Ulimboka alijikuta yupo msitu wa Mambwepande na alijivuta hadi barabarani na alikutwa na msamaria akiwa amefungwa kamba miguuni na mikononi.

Kwa mujibu wa Kamanda Kova, Dkt. Ulimboka alieleza kuwa gari yake aliiacha maeneo ya Leaders Club na watu hao waliuchukua ufunguo wake, nyaraka zake pamoja na fedha ambazo hakumbuki ni kiasi gani.

Kamanda Kova alisema ameunda jopo la wapelelezi wa fani mbalimbali chini ya Mkuu wa Upelelezi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam kwa kushirikiana na mlalamikaji mwenyewe na mashahidi walioona tukio hilo, ili uchunguzi wa shauri hilo ufanyike  na kuwaomba raia wema kutoa ushirikiano ili matukio ya aina hiyo yasijirudie.

 “Naamini kwamba watu wengi watakuwa wameguswa na tukio hili ila nawasihi watuache polisi tufanye upelelezi na waachane na minong’ono kwa kuwa sisi hatukuwa na ugomvi wowote na Dk Ulimboka wala madaktari… upelelezi utafanyika kwa makini na taarifa rasmi zitatolewa baadaye.” alisema.
Source http://www.wavuti.com/#axzz1z3Wgdo1F


No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate