Faraja Kotta
Shindano la kumsaka mrembo wa kitongoji cha Ubungo
mwaka huu "Miss Ubungo 2012" linatarajiwa kufanyika Juni 29 kwenye
ukumbi wa Land Mark jijini Dar es Salaam.
Kitongoji cha Ubungo ambacho kilikuwa kimefutwa hapo nyuma sasa kimerejeshwa na Kamati ya Miss Tanzania na waandaaji wamejipanga kurejesha kasi iliyofanywa mwaka 2004 kwa kumtoa mrembo wa taji la taifa, Faraja Kotta.
Mratibu wa shindano hilo alisema kuwa tayari warembo wanaotarajiwa kupanda jukwaani kuchuana wameshaanza mazoezi chini ya mrembo wa mkoa wa Ruvuma na Kanda ya Nyanda za Juu Kusini mwaka 2006, Beatrice Joseph.
Aliwataja warembo hao kuwa ni pamoja na Adaiya Ahmed, Mwatumu Mustapha, Suzan Stanley, Sarah Paul, Aisha Mohammed, Zena Ally, Zawadi Gulaba, Dorice Chilongola, Princess Lemmy, Mwanaidi Mohamed, Nasra Daffa, Shakila Mohamed, Darine Mmary na Mwasiti Juma.
Warembo watakaofanya vizuri na kushika nafasi tatu za juu wataiwakilisha Ubungo katika mashindano ya Kanda ya Kinondoni baadaye mwaka huu.
Chanzo cha habari ni Gazeti la Nipashe

No comments:
Post a Comment