Mwalimu
Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Naura, Ndugu Sunday G. Mshobozi ambaye
pia ndiye mwalimu pekee wa somo la Fizikia kuanzia kidato cha kwanza
mpaka cha nne.
Mwalimu
Mkuu Msaidizi wa Shule ya Sekondari ya Naura, Ndugu Mary Shirima
akifanya mahojiano na mwandishi kufahamu changamoto zinazoikabili shule
hiyo.
Nyumba pekee ya Walimu iliyoko shuleni hapo ingawa haitumiki kwa kuwa haijakamilika.
Baadhi ya wanafunzi wanaosoma shuleni hapo wakiwa katika muda wa mapumziko.
Wanafunzi wakiwa katika muda wa mapumziko wakati wenzao wa kidato cha tano wakiendelea na mitihani ya mock.
Uchunguzi
uliofanywa na Shirika la HakiElimu umegundua kuwa Shule ya Sekondari ya
Naura iliyoko katika kata ya Lemara , eneo la Njiro ni miongoni mwa
shule zenye maendeleo hafifu ya kielimu ukilinganisha na shule nyingine
za serikali na kata zilizoko katika Manispaa ya Wilaya ya Arusha.
Shule
hii iliyoanzishwa mwaka 2008 , inakabiliwa na upungufu mkubwa wa walimu
kwani kuna masomo hayajawahi kuwa na walimu toka shule hiyo ianzishwe
mfano masomo ya Chemistry, Mathematics na Book- Keeping . Pia kuna
masomo ambayo yana mwalimu mmoja mmoja mfano English, Commerce,
Literature, na Civics toka kidato cha kwanza mpaka cha nne.
Tofauti
na shule nyingine ambazo hukimbiwa na walimu kutokana na kuwa mazingira
magumu shule hii iko eneo zuri na maarufu waishio watu wenye kipato cha
juu mkoani Arusha lijulikanalo kama Njiro na kuacha maswali kuwa kama
kuna tatizo la uongozi wa shule au kuna tatizo la upangaji wa walimu
unaofanywa na serikali , hili hali shule nyingine zikiwa na walimu
lukuki.
Akielezea
sababu nyingine za kudorora kitaaluma shuleni hapa Mwalimu Mshobozi
alisema kuna mrundikano mkubwa wa wanafunzi kushinda uwezo wa shule
akitolea mfano wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza
kwa mwaka huu kufikia 307. Tofauti na malengo ya shule ya kata kusomesha
wanafunzi wa maeneo ya karibu , wanafunzi wa shule hii wanatoka katika
kata zote zilizoko manispaa hii kukiwa na umbali mrefu na kukabiliwa na
shida kubwa ya usafiri jambo ambalo pia alilielezea kuwa ni moja ya
sababu za kudorora kitaaluma kwa wanafunzi wa shuleni hapo.
Kwa
upande wake Mwalimu Mkuu msaidizi Bi Mary Shirima alisema sababu za
kudodora kitaaluma kwa shule yake ni mwako mdogo wa kielimu kwa wazazi
pamoja na watoto wenyewe akisema wengi wa wanafunzi ni kama
wamelazimishwa kuja kusoma shuleni hapo na wazazi wao hawajishughulishi
na maendeleo ya watoto wao. “ Historia ya wanafunzi waliomaliza kidato
cha nne ni tata kwani kuna waliokuwa wameolewa na wafanyabiashara mara
baada ya kumaliza darasa la saba ,ghafla wakasikia wamechaguliwa
kujiunga na kidato cha kwanza na kulazimika kuja shuleni, sasa katika
hali hiyo unatarajia nini” aliuliza Mwalimu Shirima.
Katika
mtihani wa kidato cha nne wa taifa wa mwaka jana 2011 jumla ya
wanafunzi 164 walifanya mtihani huo ambapo hakuna aliyepata daraja la
kwanza wala la pili, wanafunzi 2 walipata daraja la tatu , 24 wakapata
daraja la nne na 138 walifeli kwa kupata zero. Shule hii ilishika nafasi
ya mwisho kati ya shule 137 zilizofanya mtihani huo katika mkoa wa
Arusha. Kitaifa ilishika nafasi ya 2994 kati ya 3108 zilizofanya mtihani
huo.
HakiElimu
inatoa wito kwa Serikali kupitia mamlaka husika kuangalia upangaji wa
walimu na uchaguzi wa wanafunzi shuleni hapo. Wazazi na wakazi wa Njiro
nao wanatikiwa kuchukua jitihada za ziada kuhakikisha wanafunzi walioko
shuleni hapa wanapata elimu bora na kuelimika .Uongozi wa shule nao ni
siri ya mafanikio au kushindwa kufanya vema , hivyo uongozi wa Shule ya
Sekondari Naura uongeze jitihada kuhakikisha shule hii inafanya vema
kama shule za Kaloleni, Ngarenaro na Arusha Day . Chanzo cha habari na http://dewjiblog.com/
No comments:
Post a Comment