EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Sunday, June 17, 2012

Taifa Stars, Msumbiji kufa au kupona leo

TIMU ya soka ya Tanzania, Kili Taifa Stars, leo inashuka dimbani kuwakabili Msumbiji huku Kocha Mkuu wa timu hiyo, Kim Poulsen, akisema wana kibarua kigumu.
Licha ya ugumu huo, Poulsen alisema ushindi katika mechi hiyo ya kuwania nafasi ya kucheza fainali za Afrika, ni lazima.

Katika mechi ya kwanza iliyopigwa Februari 29, kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, timu hizo zilitoka sare ya bao 1-1.
Mechi ya leo itakayopigwa kwenye Uwanja wa Taifa wa Zimpeto jijini hapa, inatarajiwa kuwa ya ushindani mkubwa.

Poulsen raia wa Denmark, alisema wachezaji wapo kwenye morali mkubwa wa kupigania ushindi.
“Msumbiji ni timu nzuri, wanacheza kwa kasi, lakini kila kitu nimekifanyia kazi. Ninaamini tutafanya vizuri, kikubwa ni kufuata maelekezo ya kila tunachopaswa kufanya,” alisema Poulsen.
Stars ilitua hapa Ijumaa na kufanya mazoezi juzi na jana.
Naye Nahodha wa Stars, Juma Kaseja alisema ana imani kubwa wataibuka na ushindi kwani kila mchezaji yuko fiti.

“Tunataka ushindi, tumejiandaa vilivyo, tunajua Msumbiji ni wazuri, lakini wanafungika. Tuna ari kubwa ya kupigania ushindi,” alisema.
Mbwana Samatta, nyota wa kimataifa anayekipiga TP Mazembe ya DR Congo, alisema Msumbiji wanastahili heshima yao, lakini wao wanataka kushinda.

“Tunawaheshimu Msumbuji, lakini hatuwahofii kiuchezaji, tunataka ushindi. Tunajua bila ushindi tutakuwa kwenye nafasi mbaya, tutajitahidi kadiri ya uwezo wetu tushinde,” alisema.
Katika hatua nyingine, Watanzania wanaoishi nchini hapa, wamekuwa na matumaini makubwa ya Stars kushinda mechi ya leo.
Anwar Aziz, Mohamed Abballah Na John Thomas wanaofanya shughuli zao mjini hapa, walisema wanaamini Stars itashinda kwani Msumbiji haina makali kama zamani.

“Msumbiji ni timu nzuri kwenye kiungo na staili yao ya kucheza kwa kasi. Kitu muhimu kwa Stars ni umakini, jamaa wanapiga sana mashuti,” alisema Anwar.
Naye Salum Magimba anayeishi nchini hapa, alisema Stars iwe makini kwenye safu ya ushambuliaji, na kamba Msumbiji si wazuri kwenye safu ya ulinzi.

Watanzania wanaoishi hapa, wameahidi kujitokeza kwa wingi kuishangilia Stars wakati wote katika mechi hiyo itakayoanza saa 10 jioni ya hapa, sawa na saa 11 jioni ya Tanzania.
Mshindi wa mechi ya leo, atapangiwa kucheza na moja ya timu 16 zilizocheza fainali za Afrika Januari mwaka huu nchini Gabon na Guinea ya Ikweta.
              Habari na  Mwandishi maalum, Maputo wa Tanzania Daima

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate