EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Sunday, June 17, 2012

Twiga yakosa tiketi ya Afrika

HESABU za timu ya soka ya wanawake, Twiga Stars, kucheza fainali za Afrika kwa mara ya pili, jana zilitoweka baada ya kufungwa bao 1-0 na Ethiopia kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.
Licha ya kuhitaji walau ushindi wa bao moja tu kujitwalia tiketi ya kucheza fainali hizo nchini Guinea ya Ikweta, Twiga Stars wamekubali kipigo.
Kwa bao hilo moja likifungwa dakika ya 63 na Berkhatawit Girm, Ethiopia imetwaa tiketi ya fainali hizo kwa ushindi wa jumla ya mabao 3-1.
Katika mechi ya kwanza iliyopigwa wiki mbili zilizopita mjini Addis Ababa, walishinda 2-1.

Berkhatawit alifunga bao hilo baada ya kumtoka beki Fatma Khatib aliyeanguka kutokana na kushikwa na msuli.
Bao hilo lilifungwa dakika moja tu tangu Kocha Charles Boniface Mkwasa afanye mabadiliko akimtoa Fatma Mustafa na kuingia Ester Chabruma ‘Lunyamila’.
Kabla ya bao hilo, dakika za 19, 31 na 36 na 44, mabeki wa Twiga Stars walifanya kazi ya ziada kuokoa mashuti hatari ya Ethiopia.

Dakika ya 25, nahodha wa Twiga Stars, Sophia Mwasikili, nusura afunge bao kwa mpira wa adhabu baada ya Asha Rashid kuchezewa vibaya.
Katika mechi hiyo, Ethiopia walitawala kwa kiasi kikubwa wakiwalazimisha Twiga Stars kucheza soka ya kulinda zaidi kutokana mashambulizi makali.
Licha ya Twiga Stars kucharuka kipindi cha pili kwa lengo la kupata bao, Ethiopia walicheza kwa kujiamini, wakishambulia na kulinda lango lao.

Hadi filimbi ya mwisho, Ethiopia wakawa washindi wa bao hilo moja, hivyo kujitwalia tiketi ya fainali hizo.
Baada ya mechi hiyo, baadhi ya mashabiki wamelalamikia kiwango duni cha timu hiyo, wakielekeza lawama kwa benchi la ufundi.
Kwa mujibu wa wadau hao, mbali ya Mkwasa kushindwa kupanga kikosi cha ushindi, pia hata mfumo wa uchezaji, haukuwa mzuri, huku akishindwa kubadili mchezo hata baada ya kuzidiwa.

Twiga Stars: Fatma Omary, Fatma Khatib, Pulkeria Chalaji, Flora Kayanda, Sophia Mwasikili, Mwapewa Mtumwa, Amina Ally, Eto Mlenzi, Fatma Mustafa, Asha Rashid ‘Mwalala’ na Mwanahamis Omary ‘Gaucho’.
Ethiopia: Liya Shibru, Buzhan Endale, Indnshet Tsegaye, Truanche Mengesh, Henot Dengisho, Berkhatawit Girm, Eden Shiferaw, Zulka Juhad, Shetaye Sisay, Birtukan Gebrekirsto na Erehma Zerga.
                                   Habari na  Clescencia Tryphone

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate