Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, imesema Agosti 27 mwaka
huu, itatoa hukumu ya kesi ya kusambaza waraka wa uchochezi inayomkabili
Mwenyekiti wa Chama cha Democratic (DP), Mchungaji Christopher Mtikila
dhidi ya Rais Jakaya Kikwete.
Hayo yalisemwa jana na Hakimu Mfawidhi Ilvin Mugeta muda mfupi baada ya shahidi wa pili wa upande wa utetezi katika kesi hiyo ambaye ni Mpiga Picha wa Gazeti la Mwananchi, Mpoki Bukuku kumaliza kutoa ushahidi wake na Mtikila mwenyewe kumaliza kujitetea.
Hakimu Mugeta alisema anakubaliana na ushauri wa Mtikila uliosema ameamua kufunga ushahidi wake jana licha hapo awali aliahidi kuleta mashahidi wake 10 ili waje kumtetea kwasababu endapo mashahidi hao angewaleta wangezungumza mambo ambayo ameishayazungumza yeye na Bukuku na kwamba hukumu ya kesi hiyo ataitoa Agosti 27 mwaka huu.
Mtikila akimaliza kutoa utetezi wake jana alidai kuwa mashitaka aliyoshitakiwa nayo siyo sahihi na kwamba waraka aliousambaza wenye kichwa cha habari kisemacho “Kikwete kuungamiza kabisa ukristo! Ambao ndiyo umesababisha ashitakiwe , siyo wa uchochezi kwani umejaa maneno ya kumsifu Mungu.
Kwa upande wake shahidi wa pili, Bukuku akitoa ushahidi wake jana, aliieleza mahakama kuwa ni kweli kampuni yao ya uchapaji ya Mwananchi Communication Ltd ilichapisha gazeti la Mwananchi ambalo lilikuwa limenukuu baadhi ya maneno yaliyokuwa kwenye waraka huo unaodaiwa kuwa ni wa uchochezi ila hadi sasa si jeshi la Polisi au Mtikila mwenyewe alishafika ofisini kwao kuilalamikia habari hiyo kuwa imepotoshwa.
Awali ilidaiwa kuwa kati ya Januari mwaka 2009 na Aprili 17, mwaka 2010 jijini Dar es Salaam, kwa nia ya uchochezi mshitakiwa alisambaza kwa umma nyaraka zilizosema ‘Kikwete kuuangamiza Kabisa Ukristo', ‘Wakristo wasipounga upesi kuweka Mkristo Ikulu”
Katika shitaka la pili, Aprili 16, mwaka 2010 eneo la Mikocheni jijini Dar es Salaam, bila kibali alikutwa akimiliki waraka huo wa uchochezi kwa jamii.
Na Happiness Katabazi
KatabaziHappy.blogspot.com

No comments:
Post a Comment