Kiongozi mpya wa Ghana John
Dramani Mahama ameahidi kuimarisha hali ya utulivu kufuatia kifo cha
Rais John Atta Mills. Bw. Mahama mwenye umri wa miaka 53, aliapishwa saa
kadhaa baada ya Rais aliyekuwa na umri wa miaka 68 kufariki hospitalini
mjini Accra.
Upinzani wa nchini humo umesifu kasi iliyotumiwa
katika kufanya mabadiliko yaliyomkabidhi Bw.Mahama mamlaka ya kuiongoza
nchi ya Ghana na kusema kuwa ni kuonyesha kuwa Ghana ina upevu
Kidemokrasi.
Bw.
Atta Mills aliyeiongoza Ghana kuanzia mwaka 2009 alikua na saratani ya
koo na alikua na mipango ya kuwania muhula wa pili katika uchaguzi
unaopangwa kufanyika mwezi disemba.
Mwandishi wa BBC mjini Accra, Sammy Darko
anasema kuwa Rais aliyekabidhiwa wadhifa wa Rais ataongoza kama Rais
hadi wakati wa uchaguzi, ingawa haijafahamika kama atasimama kama
mgombea rasmi wa chama cha NDC(National Democratic Congress.)
Wakati wa kuapishwa mbele ya kikao maalum cha
Bunge kilichoitishwa kwa dharura, Bw.Mahama aliahidi kuwahudumia raia
wote wa Ghana. Punde baada ya kutangazwa kuwa Rais, Bw.Mahama alitangaza
maombolezi ya wiki nzima.
Kiongozi wa upinzani wa chama cha New Patriotic
Party Nana Akufo Addo amesema ameahirisha kampeni za kugombea kiti cha
Rais kwa heshima ya marehemu.
Mwenyekiti wa NPP Jake Obetsebi-Lamptey amesifu jinsi mabadiliko yalivyofanywa kufuatia kifo cha Rais.
Ingawa kulikuepo na mjadala mkubwa kuhusu afya
ya Bw.Atta Mills, suala hilo halikugusiwa rasmi, wanaserma wandishi wa
habari. Kiongozi huyo alikanusha kuhusu maumivu na kusisitiza kua katika
hali nzuri ya afya.
Kulingana na msaidizi wa Rais, marehemu
alilalamika kua na maumivu siku ya jumatatu jioni na tangu hapo hali
yake ikazidi kua mbaya.
No comments:
Post a Comment