MFUNGAJI bora wa michuano ya Kombe la Kagame, Said Bahanunzi wa Yanga
amesema kwa sasa anafikiri ni wakati wake kuitwa kikosi cha timu ya
Taifa Stars.Mshambuliaji huyo aliyejiunga na Yanga akitokea Mtibwa Sugar
ya Morogoro, aliliambia Mwananchi jana jijini Dar es Salaam:
Said Bahanunzi wa Yanga
"Nafikiri
kwa sasa tuna tatizo la ufungaji timu ya taifa, naamini nitakapopewa
nafasi nitaendeleza haya niliyofanya Kagame na timu kupata
ushindi."Aliongeza: "Siri yangu kubwa kuibuka mfungaji bora ni kwa
sababu nilimtanguliza Mungu mbele kwa kila jambo na kujituma."
"Nimezaliwa na kulelewa katika mazingira ya dini, ninamwamini zaidi mwenyezi Mungu kuliko chochote."
"Sidhani kama kweli kuna uchawi kwenye soka, ni imani potofu za watu wachache, nimejipanga kufanya vizuri zaidi na siyo kuishia hapa."
"Sidhani kama kweli kuna uchawi kwenye soka, ni imani potofu za watu wachache, nimejipanga kufanya vizuri zaidi na siyo kuishia hapa."
"Kila jambo nalofanya namtangulia Mungu, nafikiri ndiyo siri kubwa yangu kufanya vizuri kwenye mashindano ya Kagame.
Aliongeza kusema ushirikiano kati yake na wachezaji ulimsaidia kujiona yuko nyumbani na kujituma zaidi.
Bahanunzi alishawahi kuichezea Ocean View ya Zanzibar na Mtibwa Sugar ya Morogoro kabla ya kutua Yanga msimu huu.
Bahanunzi alishawahi kuichezea Ocean View ya Zanzibar na Mtibwa Sugar ya Morogoro kabla ya kutua Yanga msimu huu.
No comments:
Post a Comment