Mara kadhaa watoto mapacha
wanapozaliwa wakiwa wameungana huwa inakua kazi nzito kuwatenganisha na
wakati mwingine huwa wanafariki wakiwa kwenye zoezi la kutenganishwa na
wengine wanapoteza maisha kutokana na pesa ya hayo matibabu ya gharama
kukosekana lakini kwa Malaysia wamepata bahati wakati huu.
Kuna watoto walizaliwa April
2011 wakiwa mapacha walioungana mguuni ambapo baada ya juhudi za
Madaktari mabingwa kufanya upasuaji, wamefanikiwa kuwatenganisha hawa
malaika Muaiman na Muaimin na wakabaki kuwa hai.
Idadi kubwa ya wananchi
wakiwemo wazazi waliokua wanaifatilia habari ya watoto hawa wamejawa na
furaha baada ya kusikia hilo zoezi limefanikiwa.
Pamoja na kwamba upasuaji
umefanikiwa, ugumu ulikuwepo kwenye sehemu ya kuhifadhia mkojo mwilini
ambayo pia ilikua imeungana toka wamezaliwa, sasa hivi wapo chini ya
uangalizi wa kitaalam mpaka hali yao itakapo ruhusu kuruhusiwa kwenda
nyumbani kwa mujibu wa Star news paper.
No comments:
Post a Comment