|
Nyumba ilichomwa moto na kuvunjwa vunjwa. |
Nyumba
ya bibi Irene iliyo teketezwa siku ya jana kwa moto kwa tuuma za uchawi. Bibi
huyo ambaye amekuwa akisadikiwa kuwa na tabia ya kuwachukuwa watoto wa
majirani zake kwa nguvu ya giza ameumbuka siku ya jana baada ya mtoto mmoja aliye
potea kwa muda mrefu kwao na kutajwa kuwa alishafariki dunia kisha jana
kijana huyo ana kwa ana akakutana na ndugu yake.
Mshangao
ulitawala kwa ndugu huyo ambaye kwa ujasili alianza kumuuliza unaishi
wapi na kijana yule ndo akamwelekeza kua nipo kwa bibi mmoja anaitwa
bibi Irene na tunaishi na wenzangu wengine ambao nilikutana nao pale kwa
bibi wakiongezeka siku baada ya siku.
Bibi huyo ambaye
anatajwa kuwa mkali katika vitendo vya ushirikina, kakutwa na hilizi
kibao na mara baada ya kupata kichapo ambacho hata ivyo akikuonyesha
kumdhuru kwa licha ya kupigwa na mawe, bakora na hata vitu vingine
vigumu vya hatari hakutokwa na damu, kuvimba nundu wala kuonyesha makovu
ya majeraha mwilini mwake,
aliwambia wananchi kua watoto wengine wapo ndani na alipo ambiwa awatoe
nje alifanya mandingo yake na walio toka ni bata na kuku.
Kwa sasa bibi huyo anashikiliwa na jeshi la police jijini Mwanza kwaajili ya usalama wake.
No comments:
Post a Comment