HATIMAYE BARAZA LA MADIWANI WA JIJI
LA MWANZA WAMNG'OA MEYA MANYARERE (CHADEMA) KWENYE WADHIFA WAKE KWA
KUPIGA KURA ZA KUTOKUA NA IMANI NAYE.
Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Jiji
la Mwanza jana limeng'oa kwenye wadhifa wake Meya wa Jiji hilo
Bw.Josephat Manyerere(CHADEMA) kutokana na madai ya wajumbe wa baraza
hilo kupitia barua walioiwasilisha Mei 24 mwaka huu iliyokuwa ikimtaka
Mkurugenzi wa Jiji hilo kuitisha kikao cha dharula ili kumsomea Meya
mashitaka yake.
Madiwani waliojiorodhesha na kufikia
theluthi mbili ya wajumbe wapatao 17 kati ya wajumbe 33 wakiwa halali wa
vikao vya baraza la madiwani wa Jiji hilo ambalo ilidai ni suala la
kisheria na kanuni ya 80 za kudumu za halmashauri hiyo ambayo ipo wazi
na inasomeka .
“Halmashauri inaweza kumuondoa Mwenyekiti
au Meya madarakani kwa azimio linaloungwa mkono na theluthi mbili ya
wajumbe kutokana na sababu yoyote ya sababu hizo ni (a) Kutumia nafasi
yake vibaya(b),Kushiriki vitendo vya rushwa(c),Kushindwa
kazi(d),Mwenendo mbaya wa ukosefu wa adabu na(e) lemavu wa kimwili aidha
kiakili kwa kiasi cha kumfanya kushindwa kutekeleza majukumu yake kama
Mwenyekiti ama Meya.”ilifafanuliwa kanuni hiyo.
Mkurugenzi wa jiji la Mwanza Wilson Kabwe. |
Baada ya kukubalika kwa hoja
hiyo Mkurugenzi Bw.Kabwe aliwataka wajumbe wasiyo wa kikao hicho cha Kamati
kutoka nje ya ukumbi huku viongozi waalikwa waliongozwa na Mkuu wa Mkoa wa
Mwanza Mhandisi Evarist Ndikilo,RAS Bi Dorothy Mwanyika na Wakuu wa wilaya za
Nyamagana Bw.Baraka Konisaga na Bi.Amina Masenza wakitakiwa kubaki kwa mujibu wa taratibu za
Halmashauri.
Hatimaye baraza lilirejea kama kawaida yake baada ya kusikiliza utetezi wa Meya Bw.Manyerere ambapo katika madai kumi yaliyowasilishwa ya tuhuma zilizokuwa zinamkabili kusomewa naye kujitetea kisha ukafanyika uamuzi wa kumpigia kura za wajumbe ili kumuondoa madarakani aidha kumuacha aendelee na nafasi yake ya Umeya.
Naibu Meya wa Jiji hilo
Bw.Charles Chichibela(CHADEMA) ambaye ni Diwani wa Kata ya Mahina alitangaza
matokeo ya kura hizo za wajumbe kama ifuatavyo alisema kwamba idadi ya wajumbe
waliohudhulia kikao hicho wapatao 28 kati ya 33 ambao ndiyo halali lakini
kutokana na wengine kuwa katika majukumu mengine ya kitaifa.
Akitangaza matokeo Naibu Meya wa jiji la Mwanza Bw. Chichibela alisema kuwa madiwani
waliosema kwamba Meya Bw.Manyerere Ang’oke kwenye wadhifa huo ni wajumbe 20 na
waliosema aendelee kubaki ni wajumbe nane tu (8 ) hivyo kwa mujibu wa matokeo
hayo Manyerere hana tena sifa za kuwa Meya wa jiji la Mwanza.
Bwana Josephat Manyerere, Meya aliyetemwa na madiwani wa jiji la Mwanza kupitia kura za kutokuwa na imani naye hapa ilikuwa awali kabisa akiendesha kikao hicho kabla ya 'kuvulishwa joho'. |
Bwana Josephat Manyerere, Meya aliyetemwa na madiwani wa jiji la Mwanza kupitia kura za kutokuwa na imani naye akitoa neno la mwisho nmara baada ya 'kuvulishwa joho'. |
No comments:
Post a Comment