Paroko wa Kanisa Katoliki la Kiwanja cha Ndege, mjini Dodoma, Padre
Luyembe Sosthenes, amesema wanaotafakari kwa kina mijadala ya Bunge,
wanaona kwamba mwananchi anachukua nafasi ya tatu ama hayupo kabisa
katika mijadala hiyo.
Aidha, alionyesha kukerwa na neno kambi ya
Upinzani, ambalo alisema linaathari katika jamii kwa kuwa lugha huumba.
Aliyasema hayo wakati wa mahubiri yake, katika misa ya kwanza
aliyoiendesha katika Parokia hiyo, mjini Dodoma.
“Wanaoitafakari kwa kina mijadala ya Bunge
mnaweza kuona kwamba mwananchi Mtanzania anachukua nafasi ya tatu au
hayupo kabisa kwenye mijadala ya Bunge badala ya yeye kuwa lengo kuu kwa
sababu ya mtazamo huo wa wao na sisi,” alisema.
Alitaka kila mmoja kuwa tayari kumsikiliza
mwenzake kuthamini na kutaka kuelewa ni namna gani walifikia tafakari
hiyo ilikujenga heshima na utu.
Alitolewa mfano wakati mwingine mbunge
anatoa hoja yake baadhi huibuka na kumzomea bila ya kumsikiliza nini
anachotaka kukiongea.
Kuhusu neno Kambi ya Upinzani, ambalo
limekuwa likitumiwa kutenganisha serikali na vyama visivyotawala, Paroko
Luyembe alisema neno hilo limekuwa na uhalisia unaoathiri maisha ya
kila Mtanzania.
“Naona ugumu kuelewa kuwa kama ni utawala
wa watu na uongozi shirikishi na kama watu wote wanashirikishwa then
tuongelee kuwa kuna upinzani…Haiingii akilini.”alisema na kuongeza kuwa:
“Upinzani unajitokeza palipo na uvunjwaji
wa haki za biandamu. Lakini kama kuna kuheshimu haki za binadamu na utu
wa kila mtu, sijui kama kutakuwa na Upinzani.
Alisema katika mgawanyo wa somo la falsafa
ya lugha, kuna uchunguzi wa vitu vinne vinavyozingatiwa ambavyo ni
uasili wa maana ya neno, matumizi ya lugha, utambuzi wa lugha na
uhusiano wa lugha na ukweli lengo kuu ikiwa ni kupata mantiki ya
matumizi ya lugha au neno.
Alitaka Watanzania kufikiri neno jingine ambalo litajenga umoja wa kitanzania na kuepusha athari katika jamii.
Via
No comments:
Post a Comment