MWENYEKITI wa Jukwaa la Wahariri na Mhariri
Mtendaji wa Kampuni ya Magazeti ya Habari Corporation, Absalom Kibanda,
usiku wa kuamkia jana amevamiwa na watu wasiojulikana wakati akivuka
geti kuingia nyumbani kwake na gari yake aina ya Nissan.
Wavamizi hao walivunja kioo cha gari lake na kumchomoa ambapo walimpiga mapanga na kumjeruhi vibaya jicho la kushoto. Baada ya kufanyiwa unyama huo Kibanda alikimbizwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa ajili ya kupatiwa matibabu ambapo amelazwa kwenye chumba cha wagonjwa mahututi ‘ICU’.
(PICHA ZOTE : RICHARD BUKOS NA HARUNI SANCHAWA / GPL)
No comments:
Post a Comment