

DAR ES SALAAM, Tanzania
Benki
ya CRDB PLC imeibuka mshindi wa tenda ya kutengeneza tiketi za
elektroniki za kuingilia uwanjani iliyotangazwa na Shirikisho la Mpira
wa Miguu Tanzania (TFF), Ofisa Habari wa TFF Boniface Wambura
ameithitibishia Habari Mseto.
Kampuni
saba zilijitokeza katika hatua ya awali ya kuonesha nia (Expression
of Interest) kwa ajili ya tenda hiyo ambapo Aprili 19 mwaka huu Kamati
ya Mipango na Fedha ya TFF ambayo ndiyo Bodi ya Tenda ya shirikisho
ilipitia maombi hayo na kupitisha nne kati ya hizo.
Baadaye
kampuni hizo nne; CRDB Bank PLC, Prime Time Promotions, Punchlines
(T) Limited na SKIDATA People Access Inc. zilitakiwa kuwasilisha rasmi
tenda zao zikionesha jinsi zitakavyofanya shughuli hiyo pamoja na
gharama ya utengenezaji kwa tiketi moja.
Bodi
ya Tenda ya TFF ilikutana Julai 13 mwaka huu kwa ajili ya kupitia
tenda hizo ambapo kampuni zote nne zilifanya uwasilishaji
(presentation) wa jinsi zitakavyofanya shughuli hiyo, na baadaye kuipa
kazi hiyo benki ya CRDB.
Uamuzi
huo wa Bodi ya Tenda uliwasilishwa mbele ya Kamati ya Utendaji ya
TFF. Kamati ya Utendaji ya TFF katika kikao chake kilichofanyika Julai
14 mwaka huu iliridhia uteuzi huo wa benki ya CRDB.
Baadhi
ya vigezo ambavyo Bodi ya Tenda ya TFF iliangalia na kuipa CRDB tenda
ni, uwezo wa kufanya kazi hiyo (Capacity), hadhi yake mbele ya jamii
(Credibility) katika shughuli inazofanya na teknolojia ya kisasa
itakayotumika kutengeneza tiketi hizo.
Uamuzi
wa TFF kutangaza tenda hizo ulilenga kuimarisha udhibiti wa mapato ya
milangoni na kurahisisha mtiririko mzima wa washabiki kupata tiketi
na kuingia viwanjani.
Rais
wa TFF, Leodegar Tenga amesema: “Hatua hii ni muhimu sana, kwani
tulikuwa tukiisubiri kwa muda mrefu. Si tu itaimarisha udhibiti wa
mapato, bali pia itaondoa matatizo ya tiketi na kuendelea kujenga
Credibility (kuaminika) ya TFF. Mafanikio haya si kwa TFF pekee bali
mpira wa miguu kwa ujumla.”
Kwa
mujibu wa Wambura, CRDB imeanza mara moja mchakato wa shughuli hiyo,
ambapo tiketi hizo zinatarajia kuanza kutumika rasmi katika kipindi
cha kati ya miezi miwili na mitatu ijayo kuanzia sasa.
No comments:
Post a Comment