EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Wednesday, July 4, 2012

Dk. Ulimboka aombewa ulinzi kwenye Shirika la Kimataifa la Kutetea Haki za Binadamu la Amnesty International.

MWENYEKITI wa Jumuiya ya Madaktari Tanzania Dk. Steven Ulimboka ameombewa ulinzi kwenye Shirika la Kimataifa la Kutetea Haki za Binadamu la Amnesty International.
Vyanzo vya habari vya kuaminika kutoka ndani ya jopo la wataalam na jumuia hiyo kwa nyakati tofauti vimeliambia Tanzania Daima Jumatano kwamba wamelazimika kuomba ulinzi wa kimataifa ili kukabiliana na watu wabaya wanaotaka kumdhuru.
Vyanzo hivyo vilisema watu waliomdhuru wanataka kummaliza kabisa ili kuficha ukweli kwani kabla ya kuondoka Dk. Ulimboka alieleza ukweli wa tukio hilo hivyo wabaya wake hao wanatumia baadhi ya watumishi wa ubalozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini kuhakikisha wanampata.

“Hii ya kuomba ulinzi ni ‘latest’; Amnesty International ni wabishi lakini katika hili wameombwa naamini watakubali kumlinda… maombi yamepelekwa jana.
“Kabla ya kupelekwa Afrika Kusini Dk. Ulimboka alieleza ukweli wa tukio zima kuanzia walivyomkamata na mateso waliyompa hadi walipotaka kumzika akiwa hai.
“Wameshajulikana sasa wanatumia ubalozi wetu kutaka kupenya kwenda kumwona hospitalini ndiyo maana haisemwi yuko hospitali gani… ukweli ni kwamba usalama wa Dk. Ulimboka uko hatarini,” kilisema chanzo hicho cha kuaminika.

Bila kujua kwamba hizo ni habari chanzo hicho kiliendelea kueleza kwamba akiwa njiani kuelekea Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Dk. Ulimboka aliwataka viongozi na madaktari wengine ndani ya jumuia kupigania haki zao.
Kwa mujibu wa chanzo hicho mwenyekiti huyo wa jumuia aliwasihi waliobaki wasikubali damu yake imwagike bure, wahakikishe maslahi ya madaktari yanaboreshwa.
“Msikubali damu yangu imwagike bure; endeleeni kupigania haki zenu…,” chanzo hicho kilimnukuu Dk. Ulimboka.

Hata hivyo ilielezwa kwamba jumuia hiyo ilishirikiana na Kituo cha Sheria na Haki za Binaadam (LHRC) kuomba ulinzi huo kutoka Amnesty International.
Juhudi za gazeti hili kumpata Mkurugenzi Mtendajiwa LHRC Hellen Kijobi-Simba ziligonga mwamba baada ya kuzungumza na ofisa wa kituo hicho aliyetambulika kwa jina la Rose Mwalongo.
Mazungumzo kati ya Rose na Tanzania Daima Jumatano yalikua hivi:
Tanzania Daima Jumatano: Haloo! Samahani naomba namba ya mama Kijo Bisimba nina shida naye.
Rose: Haloo! Subiri kidogo nitakupa.
Tanzania Daima Jumatano: Asante dada Rose.
Baada ya dakika tatu ofisa huyo wa LHRC alipiga tena simu na mambo yakawa hivi:
Tanzania Daima Jumatano: Haloo dada Rose!
Rose: Haloo! Mama amepumzika hataki kupokea simu kwani kuna ishu gani kama naweza kukusaidia.
Tanzania Daima Jumatano: Ni ishu ya kiofisi kwamba LHRC imemsaidia Dk. Ulimboka kuomba ulinzi kutoka Amnesty International naomba kujua ukweli wa habari hiyo.
Rose: Sikia. Sio kila kitu kinatakiwa kupelekwa kwenye media kwa mtu kama huyu unaposema kila kitu unaweza kumsababishia matatizo lakini sidhani kama atajibu kuhusu suala hilo.
Alisema ofisa huyo na kukata simu.
Usiku wa kuamkia Juni 28 Dk. Ulimboka alitekwa, kupigwa na kutelekezwa kwenye msitu wa Pande nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam kabla ya kukutwa na msamaria mwema.
Kutokana na kipigo hicho hali ya Dk. Ulimboka iliendelea kubadilika na kuwa mbaya hadi alipopelekwa Afrika Kusini kwa vipimo na matibabu zaidi kwa kuwa baadhi ya vipimo havipo hapa nchini.

Maisha ya Dk. Deo
Awali chanzo hicho cha uhakika kilieleza kwamba hivi sasa Dk. Deo rafiki wa karibu wa Dk. Ulimboka aliyekuwa naye wakati anatekwa anaishi kwa mashaka na kuhamahama.
“Kuanzia siku ile ya tukio hadi sasa Dk. Deo anaishi kwa taabu sana kwa sababu wakati wowote na yeye wanaweza kumdhuru,” kilibainisha.
Hata hivyo juhudi za gazeti hili kumtafuta Dk. Deo kwa namba yake ya simu ya mkononi iligonga mwamba baada ya kuambiwa haipatikani.

Taarifa ya Muhimbili
Kwa mujibu wa Ofisa Uhusiano wa Muhimbili Aminiel Aligaesha licha ya utoaji wa huduma hospitalini hapo kuimarika, idadi ya wagonjwa wanaokwenda ni ndogo.
Ofisa huyo alizitaja kurugenzi zilizorejea kwenye utoaji wa huduma kuwa ni tiba, upasuaji, tiba shirikishi na uuguzi.

“Madaktari bingwa wote wamefika kazini na wanafanya kazi kama kawaida… interns (madaktari wanafunzi) 11 wamefanya kazi mizunguko wodini inafanyika kikamilifu na kliniki zote zinafanya kazi.
Alisema katika idara ya watoto, magonjwa ya nje na afya ya akili, madaktari bingwa wote nao wamekwenda kazini na wanaonana na wagonjwa kama kawaida lakini changamoto iliyopo kwao ni kuwaona wagonjwa wa nje.

“Huduma za upasuaji zinafanyika lakini sio sawa na zilivyokua kabla ya mgomo, wagonjwa ni wachache lakini wagonjwa wa upasuaji waliopo wodini wanaonwa kama kawaida.
“Huduma za uuguzi zinaendelea kutolewa kwa kiwango cha kawaida,” alisema ofisa huyo ambaye hakutaka kuulizwa maswali na waandishi.
Hata hivyo mwandishi wa habari hii alitembelea baadhi ya wodi na kuzungumza na wagonjwa ambao walidai kutoonana na madaktari badala yake wanatembelewa na wauguzi.
Baadhi ya wagonjwa waliodai kuonana na madaktari ni wajawazito waliokwenda hospitalini hapo kwa ajili ya kuhudhuria kliniki.

Kufukuza madaktari wanafunzi
Katika hatua nyingine uongozi wa hospitali ya Muhimbili umewafukuza zaidi ya madaktari wanafunzi wa vitendo 200 kwa madai ya kusitisha mazoezi yao kwa vitendo.
Akizungumza na Tanzania Daima Jumatano kiongozi wa madaktari wanafunzi Dk. Frank Kagoro alisema barua za kufukuzwa kwa madaktari hao wanafunzi zilisainiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa MNH Dk. Merina Njelekela.

Wasiwasi watanda Mwananyamala
Hali ya wasiwasi jana ilitanda katika hospitali ya Mwananyamala kutokana na kuwepo uvumi kwamba ndugu wa wagonjwa waliolazwa wamepanga kuwapiga madaktari walioshindwa kuwahudumia.
Kutokana na uvumi huo viongozi kadhaa wa Jiji la Dar es Salaam akiwemo Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadik, Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, Kamanda wa Polisi mkoa wa Kinondoni, Charles Kenyela na maofisa wengine, kuzuru hospitalini hapo na kukuta kukiwa shwari.
Akizungumza na waandishi wa habari waliotaka kujua ukweli wa uvumi huo, Katibu wa hospitali ya Mwananyamala, Edwin Bisakala, alisema uvumi huo umesababishwa na madaktari 24 waliokuwa katika mafunzo kwa vitendo ambao wamerudishwa wizarani baada ya kuanza kwa mgomo.
Kwa Upande wao baadhi ya wagonjwa waliohojiwa walisema kuwa wanaendelea kupata huduma licha ya siku za mwanzo kuzorota.
“Nipo hapa siku ya 14 leo na ninaona tofauti kuanzia siku ya kwanza ya mgomo hadi siku za hivi karibuni kwani sasa tunatibiwa na wengine wamepewa ruhusa ya kuondoka wakiwa wameshapona,” alisema Martha Lucas.
Via Tanzania Daima

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate