EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Wednesday, July 18, 2012

HALMASHAURI YA JIJI LA MBEYA LAWAFUKUZA KAZI WAHASIBU NA WATENDAJI 6 KWA WIZI WA ZAIDI YA MILIONI 35

 Meya wa Jiji la Mbeya  Athanasi Kapunga, 





HALMASHAURI ya Jiji la Mbeya, kupitia Baraza la Madiwani limewafukuza kazi  watendaji sita, wakiwemo watumishi watatu wa  Idara ya Uhasibu kwa tuhuma za kujipatia fedha isiyo halali kiasi cha shilingi milioni 35,328,314.
Watumishi waliokabiliwa na tuhuma hiyo ni Sarah Kibona Mhasibu mwandamizi,Tito Robart Mwakisole Mhasibu daraja la kwanza pamoja na  Petro Ulamso Yohana ambaye ni mlinzi.
Akitoa tamko la kuwafukuza kazi , Meya wa Jiji la Mbeya  Athanasi Kapunga, kwenye kikao cha Baraza la Madiwani mara baada ya kukaaa kama Kamati ya  kuwajadili watumishi hao, Baraza limependekeza kufukuzwa kazi kwa  watumishi hao.
Alisema, Sara Kibona pamoja na Tito Robert wanakabiliwa na shitaka (kanuni 42) kujipatia fedha isiyo halali (wizi)kiasi cha shilingi milioni 35,328,314.94 na shitaka la pili (kanuni ya 42) kushindwa kutimiza wajibu au kutekeleza maelekezo aliyopewa na mwajiri wake wa kazi na hivyo kusababisha hasara ya kiasi hicho cha fedha.
Alisema, watuhumiwa wote wanadaiwa kutumia fursa ya cheo chao kwa kushirikiana na mtumishi wa Benki ya NMB kuiba fedha za mishahara ya watumishi wasiostahili kulipwa kwa kuingiza mishahara hiyo kwenye akaunti za watu mbalimbali pamoja na za kwao wenyewe.
Aidha, Meya huyo alisema kuhusu mlinzi Petro Ulamso yeye akaunti yake inadaiwa kutumiwa na wahasibu hao kwa kuingiziwa fedha shilingi milioni 3,875,350 ambazo ni mali ya mwajiri.
 Pia mlinzi huyo anakabiliwa na shitaka la pili la kushindwa kutimiza wajibu akiwa kama mlinzi wa halmashauri ya Jiji la Mbeya na kushindwa kutoa taarifa ya kuingizwa kwa kiasi hicho cha fedha isivyo halali kwa mwajiri ili zirejeshwe serikalini.
  Baraza hili limependekeza kufukuzwa kazi kwa mthamini ardhi daraja la kwanza Joseph Ndaki kwa tuhuma za kughushi taarifa za uthamini wa ardhi ili kuidanganya serikali kwa kusudio la kujipatia manufaa binafsi kutokana na fedha ya zaidi ambayo ingelipwa kama fidia ya eneo la Ikuti na Inyala kwa ardhi na mali ambazo hazipo.
pia mtumishi huyo anadaiwa kushindwa kutimiza wajibu akiwa mtumishi wa umma, kuharibu taswira ya utumishi wa umma mbele ya jamii na kufanya vitendo vinavyodhalilisha utumishi wa umma ukishirikiana na wananchi wasio waadilifu kughushi taarifa na pia kudhalilisha mamlaka ya halmashauri ya jiji la Mbeya.
Alisema, Ndaki alikuza eneo la uthamini pasipo uhalali na kwamba hekta 72 ndizo alipaswa kuzifanyia kazi lakini yeye aliingiza hekta 190 kwa maslahi yake mwenyewe na hivyo baraza limependekeza afukuzwe kazi.Via Mbeya Yetu.com

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate