
KIUNGO
wa kimataifa wa Yanga, Haruna Niyonzima ameondoa hofu mashabiki wa timu
hiyo katika kutetea Ubingwa wao wanaoushikilia wa Kombe la Kagame
walilolichukua 2011.
Yanga walianza vibaya kutetea ubingwa huo baada ya kufungwa na wapinzani
wao Atletico mabao 2-0, mechi iliyochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini
Dar es Salaam.
Niyonzima
alisema, bado wananafasi kubwa ya kulibakisha kombe hilo la Kagame
kutokana na uimara wa kikosi chake, mashabiki wanachotakiwa ni kuendelea
kuwasapoti ili mechi zinafuata washinde.
Kiungo huyo raia wa Rwanda alisema, anaamini Kocha wao Mkuu,
Tom Saintfiet ameyaona mapungufu atakayoyafanyia kabla ya mechi
inayofuata dhidi ya Wau Salaam itakayochezwa Jumanne ya leo saa 10:00
jioni katika Uwanja wa Taifa.
Mrwanda huyo, kipigo walichokipata dhidi
ya Atletico ni cha bahati mbaya, badala yake watajipanga kwa kushinda
kila mechi watakayokutana nayo ili wafanikishe malengo yao.
mwisho
No comments:
Post a Comment