JOKETI
 Joseph (20) ameibuka kuwa mrembo wa mkoa wa Rukwa (Redd’s miss Rukwa 
2012) katika mashindano yaliyofanyika jana usiku katika  ukumbi wa 
Bomani uliopo mjini Sumbawanga.
Joketi
 ambaye pia ni mkazi wa mjini hapa, aliwashinda washiriki wenzake tisa 
kwa kushika nafasi ya kwanza katika kinyang’anyiro kilichojaa ushindani 
wa kila aina.
Jaji
 mkuu wa shindano hilo, Ismail Mpagama, alimtangaza mrembo huyo kuwa 
mshindi wa kwanza,  nafasi ya pili ikienda Asia Abdalah (19)  na mshindi
 wa tatu alikuwa Vency Edward (18).
Hata
 hivyo katika shindano hilo, ilionekana dhairi  kwamba Joketi ataibuka 
na ushindi kwani alikonga nyoyo za watu waliojitokeza ambapo kila 
alipopita jukwaani alishangiliwa na umati mkubwa wa watu waliojitokeza 
kwenye ukumbi huo .
Kwa
 mujibu wa muandaaji wa shindano hilo, Mariam Amri mshindi wa kwanza 
ajipatia zawadi ya Seti moja ya Tv na dish kutoka kampuni ya Zuku 
sambamba fedha taslimu Sh 300,000, mshindi wa pili akijivunia Sh 200,000
 na watatu akiweka kibindoni Sh 170,000 washindi wa nne na tano 
walijipatia Sh 120,000 kila mmoja huku washiriki wengine watano 
 wakiambulia kifuta jasho cha Sh 100,000.
Muandaaji
 huyo aliwashukuru wadau mbalimbali waliojitokeza kusaidia kufanikisha 
mashindano hayo huku akiahidi kuwa washindi hao watawakilisha vema 
katika mashindano yajayo ya kanda ya nyanda za juu kusini na yale ya 
 Redd’s miss Tanzania 2012 ngazi taifa.
Baada
 ya kuibuka na ushindi Joketi alisema kuwa atajitahidi kadri awezavyo 
kuibuka na ushindi katika mashindano ya kanda na kupata tiketi ya 
kuingia katika ngazi ya kitaifa ambako nako ametamba kushinda na taji 
hilo kwenda Rukwa safari hii.
Via rukwayetu.blogspot.com 
No comments:
Post a Comment