Uongozi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), umekanusha kuwepo kwa
ufisadi chuoni hapo unaodaiwa kufanywa na chuo hicho kwa kushirikiana na
benki moja mjini Dodoma katika kutafuna ada za wanafunzi.
Katika taarifa ya ufafanuzi ya chuo hicho
iliyotiwa saini na Ofisa Uhusiano wa UDOM, Beatrice Baltazary, ilieleza
kuwa habari hiyo iliyoandikwa na gazeti hili toleo lililopita, ilikuwa
na upotoshaji.
Miongoni mwa ufafanuzi huo ni kwamba
wanafunzi wote wanatakiwa kulipa gharama zote zinazoambatana na kupata
elimu chuoni hapo mara wanapoanza mwaka wa masomo.
Kwa mujibu wa ufafanuzi huo, utaratibu
uliotolewa na mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali wa kulipiwa
ada na Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu, unamlazimu mwanafunzi kusaini
ili kuthibitisha fedha kupokelewa chuoni na wale wasiosaini fedha
hurejeshwa bodi na deni hubakia kwa mwanafunzi.
“Wanafunzi wengi wamekuwa wakikaidi
kuthibitisha kupokea fedha za ada nia yao ikiwa ni kutaka kusoma bila
kulipa ada na kwa kufanya hivyo wanakuwa hawana deni katika bodi ya
Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu, hivyo basi chuo kimechukua hatua ya
kuzuia vyeti vyao hadi watakapo maliza…” ilieleza sehemu ya taarifa
hiyo.
Ufafanuzi huo umekuja wiki moja baada ya
gazeti hili kuandika malalamiko ya wanafunzi wanaolipiwa ada zao na Bodi
ya Mikopo kudai kuwa ada zao hutafunwa na chuo hicho kwa kushirikiana
na benki moja uya mjini Dodoma.
Wanafunzi hao walidai kuwa licha ya
kulipiwa ada na bodi, na wao kulipia kiasi cha asilimia walizopangiwa,
lakini uongozi wa UDOM umekuwa ukiwalazimisha kulipa tena ada kwa
maelezo kuwa hakuna rekodi zinazoonyesha kuwa walilipiwa ada na bodi.
Hata hivyo Naibu Waziri wa Elimu na
Mafunzo ya Ufundi Stadi, Philipo Mulugo, aliahidi kufuatilia suala la
bodi ya mikopo na kulitolea ufafanuzi.
Via Gazeti la Nipashe
No comments:
Post a Comment