
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za
Jamii,Mh. Dk. Faustine Ndungulile akizungumza na wajumbe wa kamati hiyo
na viongozi wakuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) wakati kamati
yake ilipofanya ziara katika makao makuu ya Shirika hilo yaliyopo
Kurasini,jijini Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF),Mh.
Deogratius Mtukamazina (kulia) akitoa salamu ya Bodi yake kwa Wajumbe
wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii iliyofanya ziara yale
leo kwenye makao makuu ya Mfuko huo yenye lengo la kujifunza mambo mbali
mbali yanayofanya na Mfuko huo.Wengine pichani ni Makamu Mwenyekiti wa
Kamati Kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii,Mh. Dk. Faustine
Ndungulile,Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii,Mh. Dk. Hussein
Mwinyi,Naibu Waziri wa Afya, Dk. Sirra Umbwa,Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi
ya Waziri Mkuu (TAMISEMI),Mh. Majaliwa K. Majaliwa.

Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii,Mh. Dk. Hussein Mwinyi
akizungumza na wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii
iliyofanya ziara yale siku ya jana kwenye makao makuu ya Mfuko huo yenye lengo la
kujifunza mambo mbali mbali yanayofanya na Mfuko huo.

Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii na Mbunge
wa Jimbo la Korogwe Vijijini,Mh. Steven Ngonyani "Prof. Maji Marefu
akisalimia wadau.

Mjumbe wa Kamati hiyo na Mbunge wa Jimbo la Nzega, Dk. Hamisi Kigwangalla nae akisalimia wadau.

Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF),Ndg.
Emmanuel Humba akitoa maelezo mafupi kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya
Huduma za Jamii.


Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii
wakifuatia kwa makini maelezo yaliyokuwa yakitolewa ukumbini hapo.

Wakurugenzi wa NHIF.


Wajumbe wa Bodi ya NHIF.

Meneja wa Idara ya Uanachama wa NHIF,Bi. Ellentruder Mbogoro
akielekeza jambo kwa Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za
Jamii walipotembelea makao makuu ya Mfuko huo,Kurasini jijini Dar es
Salaam siku ya jana.

Afisa Nyaraka wa NHIF,Erastus Msigwa akiwaonyesha Wajumbe wa
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii moja ya mafaili ya
Wanachama wa Mfuko huo yaliyohifadhiwa kwenye Masanduku ya Kisasa
yanayotumia mfumo wa Umeme.

Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii wakipata
maelezo ya namna ya uhifadhi wa Nyaraka kwa kutumia teknolojia ya
kisasa.

Sehemu ya Masanduku hayo.
No comments:
Post a Comment