EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Sunday, July 15, 2012

Taarifa kwa umma juu ya hali ya utendaji wa viongozi wa Bunge la Tanzania

Taarifa hii ni matokeo ya ufuatiliaji wa shughuli za Bunge na mijadala ya Wabunge juu ya mahitaji ya umma kwao kwenye maendeleo, uongozi, kuimarisha utawala bora, uwajibikaji wa serikali na haki za binadamu na kuimarisha usimamizi wao kwa serikali kupitia mijadala yao katika vikao vya Bunge. Taarifa hii inahusika na utendaji wa viongozi wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mwaka 2011.

Kwa Ujumla:

Kumekuwa na upendeleo wa vyama katika kujadili na kuchangia hoja na kuonekana Mh Spika na Wenyeviti wa vikao kutumia vibaya kanuni za bunge kuwadhibiti wabunge kulingana na vyama vyao. Mfano ni pale Mh Spika alipomzuia Mh Tundu Lissu kumwuliza swali Mh Mizengo Pinda juu ya mauaji ya raia mikononi mwa vyombo vya dola kwa madai kuwa kuna kesi mahakamani juu ya hoja hiyo. Pamoja na Mh Lissu kujitahidi kufafanua tofauti zilizopo kati ya kesi inayomkabili yeye na wenzake na hoja anayoiulizia, bado Mh Spika ameendelea kuizuia hoja hiyo. Kulingana na maoni ya wabunge 36, Watendaji 22, wachambuzi 11 na wananchi 48 waliohojiwa, ubora wa uongozi wa bunge  kwa mwaka 2011 ni kama ilivyo hapa chini:

NAFASI
JINA
SIFA YA KIPIMO
ALAMA WASTANI
MAONI YA WASHIRIKI
1
NDUGAI,
JOB
YUSTINO
USIKIVU KWA WABUNGE
2.5
Amejitahidi sana kukwepa upendeleo wa kisiasa na kuilinda serikali; haoneshi utashi wake kumiliki mamlaka aliyopewa na Kanuni za Bunge anapoongoza vikao.
UZINGATIAJI KANUNI
2.625
UPENDELEO WA KISIASA
2.5625
UZINGATIAJI HOJA
2.375
USHABIKI BUNGENI
3
JUMLA
KIWANGO
13.0625

WASTANI
2.6125
2
SIMBACHAWENE,
USIKIVU KWA WABUNGE
2.125
Msikivu kwa Wabunge haswa wenye HOJA zenye maslahi kwa Taifa; Amejitahidi sana kukwepa upendeleo wa kisiasa na kuilinda serikali; Anayumbishwa na makundi au siasa.
GEORGE
BONIFACE
UZINGATIAJI KANUNI
2.3125
UPENDELEO WA KISIASA
3.28125
UZINGATIAJI HOJA
2.09375
USHABIKI BUNGENI
3.4375
JUMLA
KIWANGO
13.25

WASTANI
2.65
3
MAKINDA,
ANNE
SEMAMBA
USIKIVU KWA WABUNGE
3.03125
Imara kwenye kanuni na kuzingatia hoja; Anayumbishwa na ushabiki kisiasa; si msikivu kwa wabunge.
UZINGATIAJI KANUNI
2.65625
UPENDELEO WA KISIASA
3.46875
UZINGATIAJI HOJA
2.75
USHABIKI BUNGENI
2.9375
JUMLA
KIWANGO
14.84375

WASTANI
2.96875
Anajitahidi sana kuzingatia kanuni; Anayumbishwa na makundi kisiasa; si msikivu kwa wabunge.
4
MHAGAMA,
JENISTER
JOAKIM
USIKIVU KWA WABUNGE
3.21875
UZINGATIAJI KANUNI
3.15625
UPENDELEO WA KISIASA
3.5
UZINGATIAJI HOJA
3.53125
USHABIKI BUNGENI
3.3125
JUMLA
KIWANGO
16.71875

WASTANI
3.34375
5
MABUMBA,
SILVESTER
MASELE
USIKIVU KWA WABUNGE
4.25
Haoneshi ushabiki wa wazi wa kisiasa; hushindwa kuhimili mivuto ya makundi na upendeleo wa kisiasa; Si msikivu kwa wabunge.
UZINGATIAJI KANUNI
4.25
UPENDELEO WA KISIASA
3.78125
UZINGATIAJI HOJA
3.90625
USHABIKI BUNGENI
3.25
JUMLA
KIWANGO
19.4375

WASTANI
3.8875

ANGALIZO LA VIWANGO:

                        1.00 – 1.49 = Uongozi Mzuri Sana,

                        1.50 – 2.49 = Uongozi Mzuri

                        2.50 – 3.49 = Uongozi wa Wastani

                        3.50 – 4.49 = Uongozi Dhaifu

                        4.50 – 5.0 = Uongozi Dhaifu Sana

Kwa Ujumla

Taarifa hii imeonesha mapungufu kadhaa kwenye uongozi na utendaji wa kazi wa viongozi wa Bunge na hivyo kutoa changamoto kwa viongozi wa Bunge na wabunge kuimarisha utendaji wao iwapo wangependa kutekeleza wajibu wao kwa jamii. Ni matarajio yetu kuwa wabunge watatumia taarifa hii kuimarisha mjadala wa bajeti ya 2012/13 unaoendelea, ikiwa ni pamoja na kendeha na kusimamia vema vikao na mijadala ya Bunge na kutoa changamoto kwa utendaji wa serkali kwa maslahi ya jamii.

Tunakumbusha pia kuwa bado Bunge limeendelea kutumia muda vibaya kwa wabunge kuendeleza vijembe, kebehi, shukrani, pongezi na salamu. Hata baada ya miaka miwili sasa baada ya Uchaguzi na Serikali kuundwa bado wabunge wameendelea kutoa shukrani kwa Rais, wapiga kura wao na wengineo. Matumizi haya ya muda yanapunguza mijadala na mwendelezo wa ushiriki wa wabunge kwa ufasaha.

Mapendekezo

1.    Ipo haja ya wabunge kujiangalia kwa karibu uwezo na utayari wao kujadili maswala ya maslahi kwa taifa bila kuingiza ushabiki na maslahi binafsi.

2.    Iangaliwe upya akidi ya wabunge katika kupitisha hoja (angalau iwe robo tatu na sio nusu ya wabunge kama ilivyo sasa).Hii iendane na haja kwa Mhe, Spika kujiridhisha bila kuacha shaka juu ya idadi ya kura za wabunge kwenye hoja husika, na haswa walioshiriki mjadala baadala ya kuingia kwa ajili ya kupiga kura tu;

3.    Spika atumie mamlaka na kanuni za Bunge ili kudhibiti maudhui, mantiki na maana ya mijadala ya Bunge bila kuathiri maslahi ya taifa. Katika hili Mhe Spika, Naibu na Wenyeviti wa Bunge,wana dhamana ya kuhakikisha ushabiki wa kisiasa haupati nafasi kuvuruga Bunge

4.    Tunaona ipo nafasi kubwa kwa Spika kusaidia na kuelekeza bunge ili lifanye kazi zake vizuri zaidi. Spika atumie nafasi hii baadala ya yeye kuangukia kwenye ushabiki na kuilinda serikali.

Imetolewa na Taasisi ya Raia ya Haki za Kisiasa na Mwenendo wa Bunge,

CIVIL AND POLITICAL RIGHTS WATCH
Marcossy Albanie
Mkurugenzi Mtendaji

Maneno yaliyokatika kwa juu ni haya hapa chini....
NAFASI YA 1: Amejitahidi sana kukwepa upendeleo wa kisiasa na kuilinda serikali; haoneshi utashi wake kumiliki mamlaka aliyopewa na Kanuni za Bunge anapoongoza vikao.

NAFASI YA 2: Msikivu kwa Wabunge haswa wenye HOJA zenye maslahi kwa Taifa; Amejitahidi sana kukwepa upendeleo wa kisiasa na kuilinda serikali; Anayumbishwa na makundi au siasa.

NAFASI YA 3:Imara kwenye kanuni na kuzingatia hoja; Anayumbishwa na ushabiki kisiasa; si msikivu kwa wabunge.

NAFASI YA 4:Anajitahidi sana kuzingatia kanuni; Anayumbishwa na makundi kisiasa; si msikivu kwa wabunge.

NAFASI YA 5:Haoneshi ushabiki wa wazi wa kisiasa; hushindwa kuhimili mivuto ya makundi na upendeleo wa kisiasa; Si msikivu kwa wabunge.

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate