EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Sunday, July 15, 2012

Kenya yachunguza taarifa za aliyemtesa Dk Ulimboka


SERIKALI ya Kenya imesema inazifanyia kazi taarifa za raia wake kukamatwa na kufikishwa kortini nchini kwa tuhuma za kumteka na kufanya jaribio la kumuua Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari Tanzania, Dk Steven Ulimboka.

Hatua hiyo imekuja siku moja baada ya Jeshi la Polisi kutangaza kukamatwa na kufikishwa mahakamani kwa raia wa Kenya, Joshua Mulundi  anayetuhumiwa kuhusika na tukio la  kumteka, kumpiga na kumtupa Dk Ulimboka katika Pori la Akiba la Pande nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam hivi karibuni.

Balozi wa Kenya nchini, Mutinda Mutiso, alisema kwa njia ya simu jijini Dar es Salaam jana kuwa Serikali yake itachunguza uraia na tuhuma zinazomkabili mtu huyo ili kubaini ukweli.

“Ndiyo kwanza nimewasili kutoka nje ya nchi…, nitafuatilia kwa makini kupata taarifa sahihi kutoka kwenye vyanzo sahihi na mamlaka husika za hapa Tanzania na Kenya ili kupata taarifa ya kweli,” alisema Balozi Mutiso na kuongeza: “Siwezi kueleza zaidi kwa sasa kwani itakuwa naeleza uvumi.”

MAT wadai kutoridhishwa
Wakati Balozi wa Kenya akisema hayo, Chama cha Madaktari Tanzania (MAT), kimeelezea kutoridhishwa na hatua hiyo kikisisitiza  msimamo wake wa kutaka kuundwa kwa tume huru ya uchunguzi kwa lengo la kuwabaini wahusika na kuchukuliwa hatua stahiki.

MAT pia imesema kwamba, inaendelea na mpango wake wa kuandamana, ikibainisha kuwa kesho itawasilisha barua ya kuomba kibali cha kufanya maandamano ya amani Polisi.

Imefafanua kuwa malengo ya maandamano hayo yaliyopigwa 'stop' na polisi kwa kile walichoeleza ni sababu mbalimbali za kiusalama na kwamba, madai mengi ya madaktari yamefanyiwa kazi na Serikali.

"Nisingependa kuingilia suala la kipolisi kwa ujumla wake, lakini moja ya madai yetu ni kuundwa kwa tume huru ya kuchunguza tukio la kutekwa, kupigwa na kutupwa katika Msitu wa Pande kwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari Dk Ulimboka," Katibu Mkuu wa (MAT) Dk Rodrick Kabangila aliliambia Mwananchi Jumapili jana.

TUCTA nao wamo
Katika hatua nyingine, Shirikisho la Vyama Vya Wafanyakazi (Tucta) limelipongeza Jeshi la Polisi kwa kumkamata mtu anayedaiwa kumteka na kumpiga kiongozi wa mgomo wa madaktari, Dk Steven Ulimboka.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa Tucta, Nicolaus Mgaya alisema kuwa, hatua ya kumkamata mtuhumiwa huyo inaleta matumaini ya kuwabaini watu wengine waliohusika na vitendo hivyo, jambo ambalo linaweza kurahisisha uchunguzi.
Alisema kutokana na hali hiyo, jeshi hilo linatakiwa kuendelea na uchunguzi ili waweze kuwabaini wahusika wengine na kubaini ukweli kuhusu tukio hilo ambalo limesababisha kutokea kwa hisia tofauti katika jamii.
“Tunaliomba Jeshi la Polisi liendelee na uchunguzi ili waweze kuwabaini watuhumiwa wengine na kuwachukulia hatua za kisheria,” alisema Mgaya.
Mkenya kukamatwa
Joshua Mulundi, ambaye  anatuhumiwa kumteka na kumtesa Dk Ulimboka  alikamatwa na kupandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam juzi alasiri na kusomewa mashtaka mawili na Wakili wa Serikali, Ladslaus Komanya.

Wakili Komanya alidai mahakamani hapo kuwa, Mulundi ambaye  makazi yake ni Murang'a nchini Kenya mnamo Juni 26, mwaka huu akiwa eneo la Leaders Club alimteka Dk Ulimboka.

Hata hivyo, kumetokea utata wa jina, umri wake na makazi ya mtuhumiwa huyo.

Wakati hati ya mashtaka mahakamani inasema ni Joshua Mulundi mwenye umri wa miaka 21, mkazi wa Murang’a nchini Kenya, taarifa ya Jeshi la Polisi imesema anaitwa Joshua Mahindi mwenye miaka 31 na mkazi wa Namanga nchini Kenya.

Katika shtaka la pili, Wakili Komanya alidai kuwa tarehe hiyohiyo mshtakiwa alifanya jaribio la kumsababishia kifo Dk Ulimboka kwa kumpiga katika eneo la Msitu wa Pande eneo la Tegeta jijini Dar es Salaam, kinyume cha sheria.

Hata hivyo, mshtakiwa huyo alikana mashtaka hayo akidai kuwa makosa aliyoshtakiwa nayo siyo sahihi.

Hakimu Mkazi, Agnes Mchome alimwambia kuwa hatakiwi kujibu chochote kwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza shauri hilo, isipokuwa Mahakama Kuu pekee.

Afya ya Dk Ulimboka yazidi kuimarika
Akizungumzia hali ya Afya ya Dk Ulimboka anayeendelea na matibabu nchini Afrika Kusini, Katibu Mkuu huyo wa MAT alisema kuwa, Mwenyekiti huyo wa Jumuiya ya Madaktari Tanzania anaendelea vizuri na sasa ameanza kufanya mazoezi ya kutembea.

"Taarifa tulizonazo sasa ni kwamba, hali ya Dk Ulimboka inaendelea vizuri. Ameanza kufanya mazoezi ya kutembea mwenyewe, anakula na pia anaweza kuzungumza vizuri. Amekuwa akifanya mawasiliano yeye mwenyewe na madaktari wenzake wa hapa nchini ingawa bado kuna matibabu anayoendelea nayo," alisema Dk Kabangila.

Mmoja wa Madaktari wa karibu wa Dk Ulimboka aliyepo nchini, alisema Mwenyekiti huyo wa Jumuiya ya Madaktari Tanzania amewatumia ujumbe wa kuwashukuru wanataaluma wenzake na Watanzania wote waliomchangia na kumwezesha kupata matibabu nchini humo.

Hata hivyo alisema kuwa, Dk Ulimboka ameomba suala la tukio lake la kutekwa na kuumizwa lisiwe hoja ya kujadili, badala yake madaktari na wananchi wote wajielekeze kudai haki zao, ambazo Serikali haijazipa kipaumbele.

Dk Ulimboka alisafirishwa nje ya nchi Juni 30 kwa ajili ya matibabu kufuatia jopo la madaktari lililokuwa likimtibu likiongozwa na Profesa Joseph Kahamba kudai afya yake imebadilika ghafla na pia angestahili kupelekwa nje ya nchi kwa ajili ya vipimo na matibabu zaidi ambayo hayapatikani hapa nchini.
Via www.mwananchi.co.tz

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate