EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Sunday, July 15, 2012

Lissu sasa matatani

MNADHIMU wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Tundu Lissu ameingia matatani kutokana na kauli yake kwamba Rais Jakaya Kikwete amekuwa akiteua majaji wa Mahakama Kuu wasiopendekezwa na Tume ya Utumishi wa Mahakama.

Kutokana na kauli hiyo aliyoitoa wakati akiwasilisha maoni ya kambi yake, kuhusu hotuba ya makadirio ya matumizi ya Wizara ya Katiba na Sheria, Lissu ambaye pia ni Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema) atajadiliwa na Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge.

Wakati akisoma hotuba yake, mbunge hiyo alisema majaji wanaoteuliwa na Rais hawafanyiwi ‘vetting’ (uchunguzi) na tume hiyo kuona kama uwezo na ujuzi wao unafaa kukabidhiwa madaraka ya ujaji.

Mwenyekiti wa Bunge, Jenista Mhagama ndiye aliyeamuru suala la Lissu kupelekwa katika kamati hiyo baada ya mbunge huyo kukataa kufuta kauli yake ambayo kwa mtazamo wa Serikali iliwadhalilisha majaji.

Hata hivyo, jana alipotakiwa kueleza kama ana taarifa rasmi za kuitwa kwenye kamati hiyo Lissu alisema: “Sijaitwa, lakini nina taarifa kuwa naweza kuitwa.’’

Alisema, hata wakimwita hatakuwa na jambo lolote la kuzungumza kwa kuwa Mwenyekiti wa Bunge aliyeongoza kikao hicho juzi (Jenista Mhagama), alikosea kwa kuwa ndiye aliyepaswa kumpa adhabu.
Mbunge huyo alisema  juzi aligoma kufuta kauli yake kama alivyotakiwa na Mwenyekiti kwani aliamini kuwa hata Mwanasheria Mkuu alikuwa amekosea.
Alibainisha kuwa endapo ataitwa katika kamati hiyo, atahoji kama waliomwita wamegeuka kuwa wenyeviti wa Bunge na kama si hivyo, anaamini watakosa neno la kumhoji.
Waziri wa Katiba na Sheria, Mathias Chikawe na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema kwa nyakati tofauti wakati wakijibu hoja za wabunge juzi jioni walisema: “Lissu aliwakashifu majaji bungeni, hivyo alipaswa kuomba radhi.”

Kwa upande wake Werema alimtaka Lissu kufuta kauli yake na kwamba ikiwa hatafanya hivyo basi awasilishe vielelezo vinavyothibitisha madai kwamba majaji huteuliwa bila kufanyiwa uchunguzi.

“Lissu ni mtaalamu wa sheria, lakini kauli yake  imewafedhehesha majaji na inashangaza inapotolewa na wakili machachari kama yeye,” alisema Werema.

Werema pia alimtaka Lissu kuondoa kauli yake kwa kuwataja watu ambao sio wabunge kwa kunukuu gazeti la Mwanahalisi lililowataja watu watatu kuwa wamehusika na mauaji ya Dk Steven Ulimboka.

Werema alisema iwapo Lissu hataondoa maneno yake suala hilo lipelekwe katika Kamati ya Maadili.

Kwa upande wake, Chikawe alimwombea radhi Lissu kwa majaji akisema anajua hakutoa kauli ya kuwadhalilisha majaji kwa kukusudia.

“Lissu amemtuhumu hadi Rais katika uteuzi wa majaji, hili siyo sahihi, uteuzi wa majaji hupendekezwa na tume maalumu inayohusisha majaji wazoefu ambao ndio wanapendekeza majina kwa Rais,” alisema Chikawe.

Baada ya maelezo hayo, Mhagama aliamuru Lissu kuondoa kauli yake hiyo baada ya kutakiwa kufanya hivyo na  Werema wakati akifanya majumuisho ya mjadala wa wizara hiyo.

Hata hivyo, Lissu alipopewa nafasi alisema hawezi kuondoa kauli yake kwa kuwa mchakato mzima wa kumtaka afanye hivyo haukufuata Kanuni za Bunge.

Lissu alinukuu kanuni ya 63 (1) ambayo inasema: “Bila kuathiri masharti ya Ibara ya 100 ya Katiba yanayolinda na kuhifadhi uhuru wa mawazo na majadiliano katika Bunge, ni marufuku kabisa kusema uongo  bungeni kwa sababu hiyo, mbunge yeyote anapokuwa akisema bungeni ana wajibu wa kuhakikisha kwamba anatoa kauli au maelezo kuhusu jambo au suala ambalo yeye mwenyewe anaamini kuwa ni kweli na siyo jambo la kubuni au la kubabaisha tu”.

Lissu aliongeza kuwa, Jaji Werema na Mhagama walivunja Kanuni za Bunge kwa kumtaka kuondoa kauli inayodaiwa kuwa ya uongo kinyume bila kufuata utaratibu.

Alipoulizwa kuhusu utekelezaji wa hatua hiyo jana, Mkuu wa Serikali Jaji Fredrick Werema alisema kuwa siyo lazima kwa Watanzania kufahamu hilo.
“Nilipozungumza jana (juzi) sikuzungumza na Watanzania bali nilizungumza na Bunge, hivyo siyo lazima Watanzania kufahamu jambo hilo na wala sioni sababu za kwa nini liandikwe magazetini,’’ alisema Jaji Werema.

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate