Rais Jakaya Kikwete amesisitiza kuwa kipengele cha dini hakitaingizwa
kwenye maswali ya Sensa ya Watu na Makazi kwa sababu lengo ni kutaka
kufahamu idadi ya Watanzania isaidie katika kupanga mipango ya maendeleo
ambayo haipangwi kwa misingi ya dini.
Aidha, Rais Kikwete amesema kuwa swali kuhusu dini halijapata kuwepo katika maswali katika sensa zote zilizopita.
“Halipo na halijawahi kuwepo,” alisema.
Alisema hayo jana kwenye mkutano wa wananchi katika eneo la Swaya, nje kidogo ya Mji wa Mbeya wakati akizindua mradi mkubwa wa maji kwa Jiji la Mbeya na vitongoji vyake.
“Nafahamu kuwepo madai ya baadhi ya watu kutaka swali la watu kuwa na dini gani liingizwe. Swali hili halipo na halikuwahi kuwepo kwa nia njema kabisa,” alisema na kuongeza: “Hatupangi mipango yetu ya maendeleo kwa misingi ya dini au rangi za watu bali kwa kuzingatia maeneo na shughuli, mambo ambayo hunufaisha watu wa dini zote”.
Alifafanua zaidi kwamba siyo kwamba serikali inapuuza dini za watu bali shabaha ya Sensa ni maendeleo ya wote.
Soma zaidi HabariLeo.co.tz

No comments:
Post a Comment