Chama Cha Walimu Tanzania (CWT), kimetangaza kuwa mgomo wao uko palepale
na utaanza rasmi kesho, baada ya msuluhishi aliyeteuliwa na Tume ya
Usuluhishi na Uamizi (CMA), kushindwa kuusuluhisha mgogoro kati yao na
Serikali.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Rais wa chama hicho, Gratian Mukoba, alisema kuwa mgomo huo ni halali kwani umefuata taratibu zote za kisheria zilizotakiwa, na kuwataka walimu wote nchini kushiriki bila ya woga, “Baada ya usuluhishi kushindikana na kwa kuzingatia kifungu cha 80 (1) kifungu (d) cha Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini ya mwaka 2004, walimu wanachama wa CWT, walianza zoezi la kupiga kura Julai 25, mwaka huu, na zoezi hilo lilimalizika Julai 27, na kuungwa mkono kwa asilimia 95.7 ya wanachama wote,” alisema Mukoba.
Mukoba aliongeza kuwa walimu waliopiga kura ni wale wanaofundisha katika shule za awali, msingi, sekondari maafisa walioko kwenye ukaguzi wa shule pamoja na wakufunzi wa vyuo vya ualimu na maendeleo ya jamii.
Mukoba alifafanua kwamba kwa kuwa zoezi hilo limeungwa mkono na wanachama 153,000, ambao ni zaidi ya nusu ya wanachama wote wa CWT waliopiga kura, chama hicho kimetoa notisi ya saa 48 kwa serikali kuanzia jana (juzi) mchana, na baada ya muda huo kwisha, walimu wataanza mgomo rasmi kuanzia kesho, “Walimu wote wataanza rasmi mgomo siku ya Jumatatu, kwa kubaki nyumbani bila ya kwenda kazini hadi hapo watakapoarifiwa vinginevyo na Rais wa CWT, alisema.
Aliwataka walimu wote kushiriki mgomo huo na kutahadharisha kuwa mgomo hauna uhusiano wowote na Sensa inayotarajiwa kufanyika Agosti 26 nchini kote, na kuwahakikishia kuwa kushiriki kwao hakutaathiri utumishi wao kwa kuwa umezingatia sheria.
Mukoba aliisihi serikali kuacha kugandamiza haki za walimu, kwa kivuli cha mahakama, ambao wamezingatia taratibu na sheria zote za nchi katika mgomo huo.
Walimu 8100 mkoani Kilimanjaro wameunga mgomo wa walimu kwa asilimia 95 unaotarajiwa kuanza rasmi kesho.
Hatua hiyo inafuatia baraza la CWT taifa na kupitisha maazimio ya pamoja walimu kugoma na kubaki majumbani mwao kuanzia Julai 31 mwaka huu hadi hapo serikali itakapotekeleza madai yao ya nyongeza ya mishahara kwa asilimia mia moja.
Katibu wa chama cha walimu mkoani Kilimanjaro Nathanaeli Mwandete aliwaeleza waandishi wa habari mjini hapa jana.
Alisema hakuna mwalimu atakayekwenda kufundisha shuleni na kuzitaka bodi za shule, kamati na serikali kulinda mali za shule kwa kipindi ambacho walimu watakuwa wamegoma hadi hapo serikali itakaposikiliza madai yao.
(Imeandikwa na Samson Fridolin, Thobias Mwanakatwe, Charles Lyimo na Jackson Kimambo (Moshi)/NIPASHE JUMAPILI)
VITISHO kama vya Dkt. Ulimoka
HOFU ya kutekwa, kuteswa na kupelekwa katika msitu wa Mabwepande kama ilivyokuwa kwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari nchini, Dkt. Stephen Ulimboka, imeanza kumtesa Rais wa Chama cha Walimu (CWT), Gratian Mukoba.
Akizungumza na Tanzania Daima Jumapili, Mukoba alisema amekuwa akipata vitisho vya kumzuia kushiriki kwenye mgomo walioupanga kuuanza kesho, lakini amedai vitisho hivyo havimzuii kuendelea na mkakati wa kutafuta haki za walimu.
Mukoba alisema hata kama atapelekwa katika msitu huo uliojipatia umaarufu mkubwa kwa kutumiwa kuendesha vitendo vya utesaji na uuaji, bado ukweli utabaki palepale kuwa walimu wana madai ya msingi ambayo yamekuwa yakipigwa danadana na serikali, Alibainisha kuwa watu wanaofikiri kuwa paka anaweza kugeuka simba wanajidanganya kwa sababu haki ya mtu haiwezi kuminywa na mtu yeyote hata kama ana madaraka makubwa. Unapomuona paka nyumbani kwako huwezi kumwita simba …eeh hata kama napata vitisho havitanifanya kuacha kutimiza majukumu yangu, hata kama mimi nitapata matatizo wapo watakaoendelea na kupigania haki za walimu, kwakuwa huwezi kuzuia na kumnyamazisha kila mtu, hasa katika masilahi ya taifa,” alisema.
Alisema anaamini kuwa kile kilichomtokea Dkt. Ulimboka hakitaweza kumtokea yeye kwa sababu watetezi mbalimbali na mikataba mingi ya kimataifa ipo na inasimamiwa kikamilifu na watu wasiopenda haki za watu zipotee.
Mukoba alisema serikali haina haja ya kutoa vitisho kwa walimu kuwa mgomo wao ni batili bali iueleze umma ni kesi gani na namba ngapi iliyopo mahakamani inayozuia mgomo huo, “Serikali imezoea kupiga porojo za kisiasa, porojo zao hazituzuii wala kutunyamazisha kuendelea na msimamo wetu wa kuanza mgomo kesho,” alisema.
(via Tanzania Daima)

No comments:
Post a Comment