| Manji akizungumza na wachezaji |
UONGOZI
mpya wa klabu ya Yanga leo asubuhi ulitembelea makao makuu ya klabu
hiyo mitaa ya Twiga na Jangwani, Dar es Salaam na kukutana na kuzungumza
na wachezaji.
Viongozi
hao wapya waliokuwepo kwenye msafara huo ni mwenyekiti, Yussuf Manji,
makamu mwenyekiti, Clement Sanga na wajumbe wa kamati ya utendaji,
Abdalla Bin Kleb, Mussa Katabalo na George Manyama.
Katika msafara huo, pia walikuwemo wajumbe wa kamati ya utendaji katika uongozi uliopita, Salum Rupia na Mohamed Bhinda.
Katika msafara huo, pia walikuwemo wajumbe wa kamati ya utendaji katika uongozi uliopita, Salum Rupia na Mohamed Bhinda.
Katika
kikao chake hicho na wachezaji, Manji aliwataka wawe na imani kubwa kwa
uongozi mpya kwa vile wamejipanga vyema kuhakikisha timu inapata huduma
zote muhimu na kwa wakati na pia inapata ushindi katika kila mechi
watakazocheza.
Manji aliwaeleza wachezaji hao kuwa, wanapaswa kucheza kwa ari na kujituma kwa vile matatizo yaliyojitokeza msimu uliopita hayatakuwa na nafasi katika uongozi wake.
Katika kikao hicho, wachezaji wa Yanga walionekana kuwa na furaha kubwa huku kila wakati wakipiga makofi ya kumshangilia mfadhili huyo wa zamani wa klabu hiyo.

Mbali
na Manji, viongozi wengine waliopata nafasi ya kuzungumza na wachezaji
ni Sanga na Katabalo, ambao waliwaelezea mikakati mbalimbali ya uongozi
wao.
Manji alichaguliwa kuwa mwenyekiti mpya wa Yanga mwishoni mwa wiki iliyopita baada ya kuwabwaga Edgar Chibula na John Jambele. Uchaguzi huo ulifanyika kwenye ukumbi wa Diamond, Jubilee, Dar es Salaam.

Uchaguzi
huo mdogo uliitishwa baada ya kujiuzulu kwa mwenyekiti wa zamani wa
klabu hiyo, Lloyd Nchunga, makamu wake, Davis Mosha na wajumbe wanne wa
kamati ya utendaji huku mmoja akifariki dunia.
| Manji na viongozi |
| Wachezaji wakimsikiliza Manji |
| Manji akizungumza na wachezaji |
| Manji anasalimiana na Chuji, Bin Kleb anafuatia na viongozi wengine |
No comments:
Post a Comment