Mbunge wa Iramba Mashariki (CCM),
Salome Mwambu, yupo hoi na amelazwa katika wodi ya wagonjwa mahututi
(ICU) katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), iliyopo Taasisi ya
Mifupa (MOI).
Ofisa Habari wa MNH, Aminieli Aligaesha, akizungumza na NIPASHE jana alisema ni kweli mbunge huyo amelazwa ICU tangu Jumamosi, wiki iliyopita (Julai 21).
Alisema mbunge huo amelazwa katika wodi namba mbili ya MOI, sehemu ambayo Muhimbili walipewa na MOI kuhifadhi wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalumu wa daktari.
“Tulimpokea hapa tangu Julai 21 mwaka huu na kimsingi hali yake siyo nzuri,” alisema Aligaesha.
Hata hivyo, hakueleza ugonjwa unaomsumbua mbunge huyo sababu taaluma ya udaktari hairuhusu pasipo idhini ya mgonjwa mwenyewe kukubali.
“Kimsingi taaluma ya udaktari hairuhusu daktari kutaja ugonjwa anaosumbuliwa mgonjwa labda unachoweza kufanya ni kuwasiliana na ndugu zake na mbunge ndio wanaweza wakakweleza anaumwa nini,” alisema.
Mbunge huyo awali alikuwa amelazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma kabla ya kuhamishiwa MOI.
Awali gazeti hili lilipoonana na Ofisa Habari wa MOI, Frank Matua, alisema hawezi kuzungumzia hali ya mbunge huyo kwa sababu mgonjwa huyo yupo chini ya Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Hata hivyo, habari ambazo NIPASHE imezipata kutoka katika vyanzo vyake vya habari zinaeleza kuwa mbunge huyo anasumbuliwa na shinikizo la damu na kisukari.
Katibu wa Bunge, Dk. Thomas Kashililah, amethibitisha kuumwa kwa Mwambu na kulazwa MOI.
Dk. Kashililah alisema wanazotaarifa za kuumwa kwa mbunge huyo. “Tunataarifa za kulazwa kwa Mwambu na gharama zote za matibabu zitalipwa na Bunge,” alisema.
Hata hivyo, alipoulizwa kuhusiana na hali ya mgonjwa, alisema anaendelea vizuri na kama hali yake ingekuwa si ya kuridhisha wangepata taarifa kutoka kwa uongozi wa hospitali na familia yake. CHANZO: NIPASHE

No comments:
Post a Comment