MKONGWE wa sanaa ya maigizo nchini, Jacob Steven ‘JB’ ametoa wosia kwa
rafiki zake ambao watatakiwa kuufuata siku atakapolala katika nyumba
yake ya milele.
Akizungumza na gazeti hili hivi karibuni jijini Dar,
JB alisema neno la mwisho ambalo atapenda rafiki zake walizingatie ni
kushikamana na Mungu aliye hai na kuwa na toba kila iitwapo leo.
“Hakuna
ajuaye siku ya kufa kwake. Wakati wowote nikiondoka duniani nitapenda
rafiki zangu wote washikamane na Mungu na kuwa na toba ya kweli kila
kukicha ili nao siku moja waje kuurithi uzima wa milele,” alisema JB.
Pamoja
na wosia huo kwa rafiki zake, JB amewataka wasanii wenzake kuwa wacha
Mungu siku zote ili pale umauti utakapowakuta wawe na tumaini la kuwa na
maisha mazuri baada ya kifo.
No comments:
Post a Comment