Jana tarehe 30 Julai 2012 baada ya Hotuba ya Waziri wa Afya ya Ustawi wa
Jamii kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Wizara kwa mwaka wa fedha
2011/2012 na makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka wa
fedha 2012/2013; Taarifa ya Kamati ya Huduma za Jamii kuhusu Wizara
husika na Maoni ya Kambi ya Upinzani nilitaka mjadala usiendelee mpaka
kwanza wabunge tupewe nakala ya ripoti ya Kamati ya Huduma za Jamii
iliyoshughulikia mgogoro kati ya Serikali na madaktari na kuandaa
mapendekezo ya kuboresha Sekta ya Afya nchini.
Nilifanya hivyo kwa kunukuu Taarifa ya Kamati ya Huduma za Jamii ambayo pamoja na kuwa mwezi Februari 2012 bunge lilikataliwa kujadili masuala husika mpaka kwanza kamati hiyo ikapate ukweli wa pande zote mbili na kuwasilisha mapendekezo kwa bunge, taarifa ya Kamati hiyo kuhusu bajeti iliyowasilishwa jana haikueleza chochote nini kamati ilibaini baada ya kukutana na wadau mbalimbali wa sekta ya afya wala haikueleza ni ushauri gani iliutoa kwa serikali kuupatia ufumbuzi mgogoro uliokuwepo wala haikuwasilisha bungeni mapendekezo yoyote yaliyotokana na kazi waliyopewa na bunge. Aidha, Nilinukuu pia maoni ya Kambi Rasmi ya Upinzani ambayo yalieleza bayana kuwa mwezi Juni yalitolewa majibu yasiyokuwa ya kweli bungeni kuwa Taarifa ya Kamati hiyo iliwasilishwa bungeni.

No comments:
Post a Comment