EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Friday, July 20, 2012

Meneja meli iliyozama Zanzibar akamatwa


Wananchi wakiwa kwenye foleni katika viwanja vya Maisara mjini unguja Zanzibar jana kwa ajili ya kwenda kutambua miili ya ndugu zao waliofariki kwenye ajali ya meli MV Skygat, iliyozama eneo la chumbe Zanzibar juzi. Picha na Fidelis Felix
VIFO VYA FIKIWA WATU 63, SERIKALI YATANGAZA SIKU TATU MAOMBOLEZO
Waandishi Wetu
JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linamshikilia Omari Hassan Mnkhon ambaye ni Meneja wa boti ya Mv Skagit, kwa ajili ya mahojiano baada ya kubainika kwamba kumekuwa na kasoro za kumbukumbu katika taarifa za hiyo.Wakati Jeshi hilo likimshikilia meneja huyo, hadi jana jioni saa 10:30, vikosi vya uokoaji vilifanikiwa kupata maiti 63, huku 29 kati yao ikiwa imetambuliwa majina namba za tiketi na sehemu wanakotoka marehemu.

Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova alisema jana jijini Dar es Salaam kuwa meneja wa boti Mkoa wa Dar es Salaam, anashikiliwa ili kuweza kusaidia jeshi la polisi kupata taarifa za kina kuhusu za meli hiyo.

Kova alisema tukio hilo linagusa maeneo mengi ikiwa ni pamoja na Mkoa wa Dar es Salaam ambako safari za meli hiyo huanzia na kuongeza kwamba, wanamshikilia meneje huyo baada ya kukosekana taarifa muhimu juu ya safari za boti hiyo.

“Tunamshikilia meneja wa meneja hiyo ili atusaidie kutupa taarifa za kina, kwani tukio hilo sio dogo na uchunguzi wa kina unatakiwa kufanywa,” alisema Kova na kuongeza;

“Jeshi la polisi litafanya uchunguzi wa kina kwa kushirikiana na vyombo na mamlaka zinazohusika, ili kujua chanzo cha ajali pamoja na kupata taarifa za kina za boti hiyo tangu ilipoanza safari yake,” alisema.


Maiti zilizotambuliwa

Hadi saa 10 jioni jana, maiti 63 zilikuwa zimepatikana na watu 145 kuokolewa wakiwa hai. Hata hivyo kati ya maiti hizo zilizopatikana, matiti 34 zilichukuliwa na ndugu zao.

Baadhi ya maiti waliotambuliwa pamoja na umri wao na maeneo wanayoishi katika mabano ni Anita Emanuel (42,  Kibamba -Dar es Salaam), Rukiya Issa Muombwa (miezi 2, Meli nne –Fuoni Zanzibar ), Halima Ali Khamis (23, Mtopepo- Zanzibar), Kolin Krispin (miezi 9, Kunduchi - Dares Salaam) na Rahma Ali Abdalla (miaka 52, Mfenesini - Zanzibar).

Maiti wengine ni  Said Jumanne Masanja (miaka 9, Nzega Tabora), Sauda Abdalla Omar (22, Ole Pemba), Said Juma Said (36, Arusha),  Amina Abdalla Tindwa, (miezi 6, Fuoni), Halima Ramadhani Kilimo, (53, Morogoro), Khadija Omar Ali (58), Amina Hamir Bakari (39, Chukwani - Zanzibar), Mwanahamisi Mshauri (42, Kibandamaiti),  Ali Hamdu Othman (35, Mkwajuni) na Mohamed Said Salum (40, Magomeni Mikumi - Dares Salaam).

Wengine ni Amina Ahmed Ramadhani (21, Michenzani zanzibar ), Mgeni Juma Halfani (25, Daraja Bovu), Khadija Rajab Kibune (22, Fuoni), Maua Ramadhani Feruzi (29, Mwembeladu), Hussein Ali Khamis (4, Mwanakwerekwe) na Sabiha Heri Mbarouk (25, Mgeleme, Chakechake-Pemba).

Pia wamo Halima Ali Mohamed (35, Kiwengwa- Zanzibar), Asia Juma Khamis (29, Kiembe Samaki), Yusuf Hasan Yusuf (7, Chamanzi, Dar es Salaam), Batuli Abrahmani Amir (20, Jang'ombe), Fatma Said Sultani (54, Msasani Dar es Salaam), Juma Jafari Shajak (Miezi 6, Kimaneta - Tanga) na Mohamed Ali Ngombe (41, Buguruni - Dares Salaam).

Serikali yatangaza siku
tatu za maombolezo

Kufuatia msiba huo Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imetangaza siku tatu za maombolezo kuanzia Julai 19 hadi Julai 21 mwaka huu.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Ali Mohammed Shein alisema bendera zote zitapepea nusu mlingoti na shughuli zote zinazoambatana na sherehe na burudani zimefutwa kwa muda huo lakini kazi na shughuli za Serikali zitaendelea kama kawaida

Nayo Serikali kupitia kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi ilitangaza siku tatu za maombolezo kufuatia msiba huo mkubwa uliolikumba taifa.

Lukuvi aliwaambia waandishi katika kipindi hicho cha siku tatu bendera zitapepea nusu mlingoti na shughuli za starehe zitasimamishwa ila kazi zitaendelea kama kawaida.

Rais Shein amewahakikishia wananchi na hasa waliopoteza jamaa zao kuwa Serikali itabeba gharama zote za mazishi na huduma za matibabu kwa majeruhi.

“Nimesikitishwa sana na msiba huu. Katika wakati huu si vema tukaanza kulaumiana jambo la muhimu hivi sasa  ni kuokoa maisha ya watu,” alisema Rais Dk Shein.

Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadick alisema kutokana na maagizo ya Waziri Mkuu aliyoyatoa Bungeni Mkoa wa Dar es Salaam ndio umepewa jukumu la kushuhulikia suala hilo.

Alisema kwa sasa mkoa Umepanga kutoa Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya kuhifadhi mili ya watu waliofariki katika ajali hiyo.

“Tumepanga kwamba, Hospitali ya Taifa Muhimbili ndio itahusika katika kuhifadhi miili ya watu waliopoteza maisha katika ajali hiyo,” alisema Sadick na kuongeza;

“Watu wote ambao wanajua kuwa ndugu zao walisafiri na meli hiyo wafike katika bandari ya Dar es Salaam kwa ajili ya utambuzi,” alisema na kuongeza kuwa ambayo haitatambuliwa Serikali itachukua jukumu la kuizika.

EU yatoa ndege ya uokoaji

Katika kuonyesha kuguswa na ajali hiyo, Umoja wa Ulaya (EU) umetoa ndege maalum kusaidia juhudi za utafutaji na uokoaji katika eneo la ajali.

Balozi wa Uingereza hapa nchini  Diane Corner aliwaambia waandishi wa habari mjini Zanzibar kuwa wameamua kutoa msaada wa ndege hiyo ambayo iliwasaili Zanzibar usiku wa kuamkia Julai 19, kitokea katika visiwa vya Ushelisheli.

“Hii ni ndege maalum ambayo kazi yake ni kuratibu na kubainisha eneo ambalo kuna watu na inawasiliana na waokoaji walioko majini ikiwa angani,” alisema Balozi Corner.

Alifafanua kwamba, Umoja wa Ulaya unaendelea kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ)  katika kazi ya uokoaji, lakini pia Umoja huo upo tayari kutoa msaada wowote utaohitajika.

Kwa upande wake, Balozi wa Marekani nchini, Leahant Alfonso alisema Serikali yake imetoa msaada wa dawa kwa ajili ya watu waliojeruhiwa katika ajali hiyo.

Balozi Alfonso aliipongeza SMZ kwa kuchukua hatua haraka kukabiliana na maafa hayo.

“Nawapa pole watu wa Zanzibar kwa msiba huu, nimesikitishwa na kuhuzunishwa sana, hasa nilipoziona maiti saba za watoto wadogo. Moyo wangu umeumia sana,” alisema huku akibubujikwa machozi.

Wabunge wachangia maafa
 
Katika hatua nyingine, wabunge wote watakatwa posho ya siku moja kuchangia maafa ya kuzama kwa boti  hiyo huku  Bunge likiahirishwa kwa siku moja kuomboleza maafa hayo.

Posho hizo za wabunge zitawezesha kupatikana kwa Sh24.6 milioni kutoka kwa Wabunge wa sasa 352 ambao kila mmoja atachagia Sh70,000.

Spika Anne Makinda jana asubuhi aliahirisha shughuli za Bunge kwa siku moja na kutangaza kuwa, Kamati ya Uongozi ya Bunge katika kikao chake jana asubuhi, iliamua zikatwe posho za siku moja na fedha hizo zitatolewa kama rambirambi kwa ndugu wa watu waliopoteza maisha katika ajali hiyo.



Wakizungumza baada ya ajali hiyo, baadhi ya wabunge waliitupia lawama Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA), kwa kile walichodai kuwa ilishindwa kutoa taarifa ya tahadhari kwa watumiaji wa usafiri wa majini.

Mbunge wa Mtera (CCM), Livingstone Lusinde alisema mamlaka hiyo inabeba lawama kwa kushindwa kutoa ushauri kwa vyombo husika na badala yake wanafanya kazi ya kutabiri mvua tu.

“Wale jamaa hawafai kabisa, matatizo yote wanatakiwa kubebeshwa wao kwa kuwa hawakuweza kutoa ushauri juu ya nini kingetokea mbele ya safari,’’ alisema Lusinde.

Mbali na Mamlaka ya Hali ya hewa, lakini mbunge huyo alitaka pia wakaguzi wa vyombo vya majini kuwajibika kwa kushindwa kukagua uimara wa vyombo hivyo.


Kwa upande wake Mbuge wa Viti Maalumu (CCM), Martha Mlata alisema tukio la kuzama kwa meli hiyo alilipokea kwa masikitiko lakini akasema “ni kazi ya Mungu.’’

Mlata alisema tangu juzi yeye pamoja na wabunge wengine wako katika maombi mazito ya kutaka Mungu awanusuru majeruhi na kuwapa nguvu ya ujasiri waokoaji ili wafanya kazi yao kwa moyo wa kujituma zaidi.

“Unajua tunafanya mambo tangu tulipopata taarifa za ajali hiyo na hadi sasa tunatakiwa kuendelea kufanya maombi hayo kwa ajili yha ndugu zetu, naamini mkono wa Mungu hautapungukia kitu,’’alisema Mlata.


Ushuhuda wa mabaharia, waokoaji

Akizungumzia  ajali hiyo, mmoja wa waokoajii binafsi, waliofika katika tukio hilo alisema boti hiyo imebinuka ikiwa mgongo juu.

Mmoja wa wahanga aliyenusurika katika ajali hiyo, Hassan Khatib alisema tangu waliondoka Dar es Salaam mnamo  saa 6:00 mchana juzi, hali ya bahari ilikuwa mbaya kwa sababu kulikuwa na mawimbi makubwa baadaye meli ilizidiwa na kupoteza mwelekeo.

Alisema baada ya hapo ililala upande na kisha ilibinuka na yeye kutupwa kwenye maji na akawa hana kitu cha kushika ndipo alianza kuogelea na kufanikiwa kushi ubao na kuogelea nao.

Alisema huduma uokoaji zilichelewa kufika ila mara baada ya ajali ilifika ndege na kuzunguka katika eneo la tukio na kuondoka na baada ya  saa kadhaa vilifika vyombo ukoaji.

TMA watoa kauli
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Huduma za Utabiri Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA), Dk Hamza Kabelwa alisema kuwa, kupitia ofisi yao iliyopo bandarini Dar es Salaam walitoa taarifa kwenye vyombo vya usafiri wa majini juu ya upepo mkali uliokuwa ukivuma baharini kwa kasi ya kilometa tatu kwa saa kuanzia saa 2:00 asubuhi hadi saa 5:00 asubuhi.
“Tulipogundua hali hiyo tulitoa taarifa kwa wahusika wa vyombo vya usafiri wa majini tu,” alifafanua Dk Kabelwa.
Meli ya Skagit ilitengenezwa mwaka 1989 nchini Marekani na ilikuja nchini 2008.
Shahihisho
Jana gazeti hili lilichapisha kwa makosa kuwa meli iliyozama inaitwa MvSkad badala ya Skagit.

Habari hii imeandikwa na Boniface Meena, Habiel Chidawali, Dodoma, Salma Said, Zanzibar
Aidan Mhando, Pamela Chilongola na Victoria Mhagama, Dar 

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate