EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Friday, July 27, 2012

Mkurugenzi wa Makumbusho ya Taifa, Jackson Kihiyo amesimamishwa kazi

Mkurugenzi wa Makumbusho ya Taifa, Jackson Kihiyo amesimamishwa  kazi kwa muda usiojulikana  ili kupisha uchunguzi dhidi ya tuhuma zinazomkabili.

Akizungumza kuhusu hatua hiyo, Mkurugenzi huyo alisema  aliitwa na mkubwa wake wa kazi, ambaye ni Katibu Mkuu  Wizara ya Maliasili na kufahamishwa kuwa amesimamishwa kazi ili kupisha uchunguzi kwani kuna tuhuma kuhusu utendaji wake katika ofisi hiyo, “Baada ya kupewa taarifa hizo, juzi (jumanne) nilikabidhi ofisi na hivi sasa nipo nyumbani. Cha muhimu ni kuwa sijafukuzwa ila nimesimamishwa na ninaendelea kupata mshahara wangu kama kawaida haid pale watakapomaliza huo uchunguzi wao,” alisema Kihiyo

Kihiyo alisema, hakutaka kumhoji mkuu wake wa kazi kuhusu tuhuma zinazomkabili kwa sababu alitaka wawe huru na wafuatilie kwa kina bila kuingiliwa, hivyo hadi sasa hafahamu kilichomsimamisha kazi, “Najua wakimaliza watanijulisha, sina mashaka yeyote kwa sababu najua hakuna kibaya nilichofanya, nikiwauliza uliza watadhani ninataka kuwaingilia katika uchunguzi wao. Waache wafanye uchunguzi kwa utaratibu na kwa uhuru wakimaliza watanieleza kilichopatikana,” alisema Mkurugenzi huyo.

Chanzo cha habari kutoka katika ofisi hiyo kilichozungumza kwa masharti ya kutotajwa jina lake kilibainisha kuwa mkurugenzi huyo amefukuzwa baada ya wafanyakazi kupeleka malalamiko kwa katibu mkuu, Maimuna Tarishi, ikiwemo utata katika ukusanyaji wa mapato na  maslahi ya wafanyakazi, “Mkurugenzi alitoa amri ya kukusanya mapato katika vituo vyote na kisha mapato hayo katika akaunti ya makao makuu. Hili jambo lilizua maswali kwa sababu tutapelekaje mapato yote makao makuu, vituo vitajiendesha na nini? Lakini lingine ni maslahi duni ya wafanyakazi, hatujaboreshewa mishahara kwa muda mrefu,” kilisema chanzo hicho.

Chanzo hicho kiliongeza kuwa malalamiko mengine kuhusu  utendaji wa mkurugenzi huyo ni kitendo cha Ofisi kutumia Menejimeti ya Umma kumuadhibu mfanyakazi badala ya kutumia Kamati ya Nidhamu jambo alilodai linasababisha uonevu mkubwa kwa wafanyakazi.

Shutuma nyingine dhidi ya Kihiyo ni upandishwaji wa vyeo  kwa wafanyakazi usiozingatia sifa stahiki na kutokuwepo mipango endelevu ya mafunzo kwa wafanyakazi.

Kabla ya Kihiyo, Mkurugenzi wa Makumbusho alikuwa ni Nobert Kayombo, ambaye alifariki Novemba 30, 2010.

Florence Majani
MWANANCHI

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate