BOTI tatu zinazofanya safari za Dar es Salaam, Unguja na Pemba
zimefutiwa usajili kufanya kazi ya kuchukua abiria pamoja na mizigo
katika bandari ya Zanzibar kutokana na kutofikia viwango vya usalama.
Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usafiri baharini Zanzibar, Abdallah Hussein Kombo amewaambia waandishi habari huko ofisini kwake Malindi mjini Zanzibar.

Kombo alizitaja boti hizo kuwa ni Seagull, Mv Sepide na
Mv Karama na kusema kuwa vyombo vyote hivyo baada ya kupokea barua rasmi
ya ufutaji huo zitapewa muda wa mwezi mmoja kwa wamiliki wa vyombo
hivyo kuziondoa katika Bandari ya Malindi.Kombo alisema Boti hizo
zimefungiwa kwa mujibu wa sheria ya Zanzibar 2004 kifungu 17 (1) ambayo
inasema, “Msajili wa meli anayo haki kuifuta meli yoyote ile ambayo
haina vigezo vya usalama wa abiria pamoja na uchakavu.
"Tunafanya oparesheni kabambe kuhakikisha meli zote ambazo hazina kiwango zinaondoka katika bandari yetu,” alisema Kombo ambaye ni Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usafiri baharini Zanzibar.
Kombo alisema kwa mujibu wa sheria hiyo vyombo hivyo haviwezi kusajiliwa tena katika bandari ya Zanzibar."Vyombo hivi ambavyo tunamevifungia hatutovirusu tena,” alisema Kombo.
Pia kaimu huyo alifahamisha kuwa mbali na kuzifutia boti hizo, Ofisi yake imeisimamisha boti ya Kilimanjaro 3 kutokana na vyombo vya uokozi vilivyomo pembeni kupitwa na wakati."Na boti hii hatutoiruhusu hadi watakapokamilisha urekebishaji wa mapungufu ambayo tumewaambia,” alifahamisha Kombo.
Sambamba na hilo pia Mamlaka hiyo imeipunguzia Meli ya Serengeti kuchukua abiria 800 hadi 350 kutokana na kile alijodai imechoka na tani za mizigo kutoka 100 hadi 50."Meli yoyote kama haitakidhi kiwango ambacho tunakitaka bandarini haitofanya kazi katika Visiwa vyetu kwa usalama wa raia wetu” alishishitiza Kombo.
Hatua hiyo imekuja baada ya meli ya Mv Skagit kuzama katika ksiwa cha Chumbe ikiwa njiani kuelekea Zanzibar ikitokea DarSalam na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 85.

No comments:
Post a Comment