EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Friday, July 13, 2012

MREMBO BORA WA MISS SINZA 2012 KUPATIKANA LEO HII, TWANGA KUWASHA MOTO

 Mwalimu wa warembo wa shindano la kumsaka Miss Sinza 2012, Mwajabu Juma, akitoa maelekezo kwa warembo hao wakati wa mazoezi yao ya mwisho kujiandaa na shindano hilo litakalofanyika SIKU YA LEO katika Ukumbi wa Mawela Social, karibu na Vatcan Hoteli, Sinza. Shindano hilo litasindikizwa na burudani kabambe na shoo ya kufa mtu kutoka kwa Bendi ya African Stars, watakaokuwa wakitambulisha pia baadhi ya nyimbo zao mpya kwa mara ya kwanza, pamoja na msanii wa Vichekesho kutoka kundi la Ze Commedy linalorusha michezo yake kupitia Televisheni ya Chanel 5, Masawe Mtata, ambaye pia atakuwa akitambulisha video ya wimbo wake mpya uitwao Uongo Kweli.
 Warembo hao wakiwa katika mazoezi yao ya pamoja ya shoo ya ufunguzi, jana jioni ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mwisho kuelekea shindano lao litakalofanyika kesho kwenye Ukumbi wa Mawela Social, karibu na Vatcan Hotel.
 Warembo hao wakiwa katika mazoezi yao ya pamoja ya shoo ya ufunguzi, jana jioni ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mwisho kuelekea shindano lao litakalofanyika kesho kwenye Ukumbi wa Mawela Social, karibu na Vatcan Hotel.
 Warembo hao wakiwa katika mazoezi yao ya pamoja ya shoo ya ufunguzi, jana jioni ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mwisho kuelekea shindano lao litakalofanyika kesho kwenye Ukumbi wa Mawela Social, karibu na Vatcan Hotel.
 Warembo hao wakipozi kwa picha ya pamoja baada ya kumaliza mazoezi yao.

Warembo hao wakipozi kwa picha ya pamoja baada ya kumaliza mazoezi yao.
MASHINDANO ya kumsaka mrembo bora waKitongoji cha Sinza, Redds Miss Sinza 2012 yatafanyika LEO (Ijumaa) kwenye ukumbi wa Mawela Social Hall (Ten Star Lounge) uliopo karibu na hoteli ya Vatican City.
 
Mashindano hayo yatashirikisha jumla ya warembo 14 wanaowania taji la kituo hicho pamoja na kuiwakilisha kitongoji cha Sinza kwenye mashindano ya Kanda ya Kinondoni na baadaye Miss Tanzania.
Mbali ya taji (crown) na nafasi ya kuiwakilisha Sinza katika Mashindano ya Kanda ya Kinondoni, pia mshindi wa kwanza katika shindano hilo atajinyakulia kitita cha sh. 500,000/=  katika mashindano hayo yatakayopambwa na bendi ya African Stars “Twanga Pepeta International’ ambao watakuwa wakitambulisha baadhi ya nyimbo zao mpya na Msanii wa vichekesho wa kundi la Ze Comedy la Chanel 5, Masawe Mtata, atakayekuwa akitambulisha video na wimbo wake mpya wa Uongo Kweli.
 
Akizungumza na mtandao huu, Mratibu wa mashindano hayo kutoka kampuni ya Calapy Entertainment, Majuto Omary, alizitaja zawadi nyingine kuwa ni shs 400,000 kwa mshindi wa pili, sh. 300,000 kwa mshindi wa tatu . Mshindi wa nne na wa tano watapata sh. 150,000 kila mmoja na waliobaki watapata sh. 100,000 kila mmoja kama kifuta jasho.
Aidha Majuto, aliongeza kuwa mbali ya kutembea jukwaani kwa ‘catwalk’ kwa warembo hao, pia kutakuwa na shindano la kusaka vipaji ambapo warembo watachuana  ili kumpata Mafoto Miss Talent Sinza 2012, ambapo mshindi atapata sh. 50,000 kutoka mtandao wa sufianimafoto.blogspot.com.
 
“Maandalizi yamekamilika na viingilio vitakuwa ni sh. 10,000 kwa viti vya kawaida na sh. 25,000 kwa vitu Maalum (VIP), tumeandaa shoo fupi na ya aina yake ili baadaye mashabiki wa fani ya urembo wa kitongoji cha Sinza wapate fursa ya kusugua kisigino na bendi ya Twanga Pepeta,” alisema Majuto.
Majuto aliwataja Warembo wanaowania taji hilo kuwa ni pamoja na Mariam Miraji, Naima Mohamed, Lulu Ambonela, Maria John, Judith Sangu, Eva Mushi, Vailet John na  Esther Mussa.
Warembo wengine ni Christina Samwel, Nahma Said, Aisha Ramadhan, Nancy Musharuzi, Brigitter Alfred na Merina Mushi.
Shindano hilo limedhaminiwa na Redds Premium Cold, Dodoma Wine, Gland Villa Hotel, Clouds FM, mtandao wasufianimafoto.blogspot.com, Brake Point, Fredito Entertainment, Screen Masters,  Lady Pepeta na flexi.

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate