Mweka
Hazina wa Chama cha Mapinduzi Zanzibar, Mansoor Yussuf Himid amesema
yupo tayari kunyanganywa kadi ya chama hicho lakini hataregeza msimamo
wake juu ya kuitetea Zanzibar katika Muungano.
Kauli ya Mansoor imekuja siku chache baada ya chama hicho wilaya ya mjini kutoa maamuzi ya kuwataka viongozi wenye kupingana na msimamo wa chama kurejesha kadi za chama hicho au kuacha tabia hiyo mra moja.
Akizungumza na Idhaa ya Kiswahili ya Radio ya Ujerumani (DW), Mansoor alisema kamwe hawezi kuogopa vitisho vinavyotolewa na watu wenye kujipa madaraka na udikteta ambao hawataki mabadiliko wala mawazo tofauti.
“Nimesema hayo tokea muda mrefu chama hiki kimetukuka na kina heshima na maadili yake ni baadhi ya watu wanataka kutuziba midomo lakini Mimi sijasema leo nimesema tokea 2008-2009 juu ya msimamo wangu juu ya mfumo wa muungano na leo naendelea kusema tena hata ikipidi kunyanynganywa kadi mimi narejea tena kuwa mfumo huu wa serikali mbili sikubaliani nao na nitaendelea kusema ahivyo hivyo siwezi kubadilisha maoni yangu leo baada ya kuwa na msimamo miaka yote hayo” alisisitiza Himid ambaye ni Mjumbe wa NEC.
Bofya kifute cha pleya kusimiliza mahojiano hayo au soma zaidi taarifa hii kwa maandishi kwye blogu ya Salma Said - ZanzibarYetu.wordpress.com

Hata hivyo alisema zama za kusema tunakwenda na fikra za mwenyekiti umepitwa na wakati na sasa jamii kubwa inakwenda na vijana amabo wanataka mabadiliko nchini hivyo aliwashauri wana CCM kuwaachia watu watoe maoni yao kwa uhuru kwani katiba tayari imetoa uhuru huo hivyo CCM hawawezi kuwa juu ya sheria.
“Hii nchi sio ya CCM peke yake, hapa kuna CUF, kuna CHADEMA na pia kuna vyama vyengine lakini wengine hawana hata vyama sasa hatuwezi kuendelea na watu ambao hawataki kuwa na mabadiliko wenye mawazo mgando …zama hizo zimeshapitwa na wakati wakati wa kwenda na fikra za mwenyekiti umekwisha” alisema Mansoor ambaye ni Waziri aisye na Wizara mmaalumu.
Jana akihojiwa na DW, Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye alisikika akisema kwamba viongozi wanaokwenda kinyume na madili ya chama chao watatakiwa kwenda kujieleza katika vikao na iwapo watathibitika wamekwenda kinyume basi watanyanganywa kazi au kufukuzwa.
Akijibu suala hilo Himid alisema kuwa Nape hawezi kugawa matabaka wanachama wa CCM, wale wa Tanzania Bara na Zanzibar kwani wote ni wanachama wanahaki sawa mbele ya sheria na katika CCM.
“Sisi Watanzania hatuna uhuru, yeye amegawa kwa utabaka, sisi ni watu wazima tuna haki na uhuru, Nape hawezi kutwambia sisi watu wazima kwamba tukasema anayotaka yeye, ule wakati wa ndio Mwenyekiti haupo kila mtu ana haki yake kutoa maoni na hata Tume ya Jaji Warioba inasema hivyo” Alisema Himid. Na kuongeza kwamba.
“Mimi naichukulia kuwa hii ni njama ya kutaka kuwaziba midomo Wazanzibari, hatujakiuka miongozo wala sheria tutaendelea kusema kutaka mabadiliko ya muundo wa Muungano, hii nchi asilimia kubwa ni vijana na vijana wanataka mabadiliko na hilo haliwezi kukwepwa” Aliongeza.
Alisema hakuna mtu mwenye nia ya kuvunja Muungano, lakini ni lazima kukawepo kwa Muungano wenye maslahi ambayo hautakuwa na kero na ndio maana wamekuwa wakitoa maoni ya kutaka mabadiliko ya muundo na sio kuvunja.
“Mimi pia nakubali muungano una manufaa, lakini sikubaliani na mfumo wa Muungano na ndio maana tunasema kwa mfumo huu sebu (sitaki)” alisema Mweka Hazina wa CCM Zanzibar.
No comments:
Post a Comment