Jeshi la polisi mkoa wa Kinondoni linawashikilia zaidi ya watu 13
akiwemo Mwenyekiti wa Mtaa wa Madale, Alex Mbuya, baada ya kudaiwa
kuhusika na vitendo vya uvamizi wa mashamba ya watu katika maeneo ya
Wazo na Madale, jijini Dar es Salaam.
Kamanda wa polisi wa mkoa huo, Charles Kenyela, aliliambia NIPASHE Jumapili, kuwa jeshi lake linatarajia kuwafikisha watu hao mahakamani siku yoyote kuanzia Jumatatu ijayo.
Kenyela alisema kushikiliwa kwa watu hao kunafuatiwa ofisi yake kupokea malalamiko mengi ya wamiliki wa mashamba yao kuvamiwa na watu wengine kwa kujengwa au kuuzwa.
Alisema wanamshikilia mwenyekiti huyo kutoka juzi kwa kuwa ndiye mwenye dhamana ya eneo hilo na kwamba inadaiwa kuhusika na uvamizi huo wa mashamba ya watu. Alisema watu wengine wanaoshikiliwa ni wenye nafasi mbalimbali na kwamba kwa sasa wanaendelea kuwahoji, "Yapo malalamiko mengi ofisi yangu imeyapokea kuhusiana na uvamizi wa maeneo yao ambapo, watu hawa imefikia hatua wamekuwa wakiharibu mipaka ya mashamba ya watu ili kupoteza ushahidi," alisema.
Kenyela amewatahadharisha wananchi waliopo eneo hilo na mengine ambao wamevamia maeneo ya watu kuondoka mara moja kwa sababu wanatarajia kufanya operesheni hivi karibuni, "Niwaombe wananchi ambao wamevamia mashamba ya watu kuondoka mara moja wasitake shari ya kupambana na dola, hatutaki tuwaondoe kwa kutumia nguvu, waondoke wenyewe."
via NIPASHE

No comments:
Post a Comment