EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Friday, July 27, 2012

NIDA yawatia mbaroni 3 walitapeli kwa kudai fedha katika zoezi la Vitambulisho vya Taifa

Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), imewakamata watu watatu na kuwafikisha polisi kutokana na makosa ya kuomba fedha kwa watu wanaokwenda kujiandikisha vitambulisho vya utaifa.

Akizungumza na MTANZANIA, Ofisa Habari wa Mamlaka hiyo, Thomas William, alisema watu hao walikamatwa katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam, yakiwemo Bunju, Mabwepande na Yombo Kilakala, “Hawa watu wamefanya mambo ya kihuni…tumewakamata na tumewafikisha kwenye vituo vya Polisi, tunataka sheria ichukue mkondo wake. Hawa watu tumewakamata baada ya kupata taarifa kutoka kwa wananchi, naomba wananchi waendelee kutupa taarifa kwani bila wao hatutajua uchafu unaofanyika katika vituo vya kujiandikishia,” alisema William.

Akizungumzia suala la msongamano kwenye vituo vya kujiandikishia, William alisema wameamua kuongeza idadi ya maofisa usajili katika vituo, “Tumeongeza idadi ya maofisa usajili katika maeneo ..tumeongeza jumla ya wasajili 240…lakini pia mtu anayejua kusoma na kuandika atapewa fursa ya kujisajili mwenyewe kwa kupewa fomu, lengo ikiwa ni kupunguza foleni,” alisema William.

Akitoa ufafanuzi kuhusu kuongeza muda wa kujiandikisha, alisema hivi sasa hawawezi kusema kama wataongeza muda hadi zoezi hili, litakapofika mwisho, “Kwa sasa ni mapema kusema kama tutaongeza muda, tutakapofika tarehe ya mwisho ndiyo tutaona…lengo ni kuandikisha wananchi wote, kwa hiyo tutaona ifikapo mwisho,” alisema William.

Wakati huo huo, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo, Dickson Maimu, alisema mamlaka ina vituo 451 na watendaji 2,279 na wataendelea kuongeza pale itakapohitajika, “Tuna vituo 451 Dar es Salaam, huku watendaji wakiwa 2,279, lakini NIDA tumeongeza watendaji wengine 240 wiki hii na kufanya idadi hiyo kuwa ya kutosha kwenye vituo vyetu,” alisema Maimu.

Kwa mujibu wa Maimu, zoezi la uandikishaji wa Vitambulisho vya Taifa, limelenga kutengeneza daftari kuu la kudumu la utambuzi wa watu.

Hata hivyo, Mjumbe wa Serikali za Mtaa Sinza C, Fredriki Kapufi, amesema licha ya kuwa na mwamko mzuri wa wananchi, lakini kuna watu wengi bado hawajafikiwa.

Aliishauri Serikali kutoa elimu kwa wananchi juu ya umuhimu wa vitambulisho vya taifa, kwani bado kuna changamoto kwa baadhi ya wananchi.

Imeandikwa na:
Elizabeth Mjatta, Otilia Paulinus na Mariam Kibondei
Wa gazeti la MTANZANIA

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate