STATE HOUSE ZANZIBAR
OFFICE OF THE PRESS SECRETARY
PRESS RELEASE
Zanzibar
27.7.2012
RAIS
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dk.
Ali Mohamed Shein, ameiagiza Wizara ya Nchi Afisi ya Rais Fedha, Uchumi
na Mipango ya Maendeleo kuandaa utaratibu wa kupata fedha ndani ya wiki
moja kwa ajili ya kununua meli kubwa mpya ya abiria wapatao 1000 na
yenye uwezo wa kuchukua mizigo ya tani 100.
Dk. Shein ametoa agizo hilo leo wakati alipokuwa na mazungumzo na uongozi wa Shirika la Meli pamoja na Wajumbe wa Bodi ya Shirika hilo ambapo pia kikao hicho kilihudhuriwa na uongozi wa Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano na Wizara ya Nchi Afisi ya Rais Fedha, Uchumi na Mipango ya Maendeleo.
Katika kikao hicho maalum Dk. Shein ameiagiza Wizara hiyo kutafuta fedha hizo kutokana na vianzio vya ndani au nje ya nchi ama kutokana na taasisi zinazohusiana na mambo ya fedha.
Alieleza kuwa katika kipindi kisichozidi miezi miwili ujumbe maalum uende kwa Kampuni zinazotengeneza meli nchini Korea Kusini, China au Japan kwa ajili ya kuwasilisha fedha za utangulizi kwa ajili ya ujenzi wa meli hiyo.
Mapema uongozi wa Shirika la Meli, ulimueleza Dk. Shein kuwa kwa kawaida ujenzi wa meli yenye ukubwa huo, huchukua mwaka mmoja kukamilika.
Kikao hicho ambacho kilikuwa na lengo la kuangalia mwelekeo na Mipango ya Shirika la Meli pia, kilijadili hali halisi ya meli za Shirika la Meli na baadae kujadili masuala ya ununuzi wa meli mpya itokayowaondoshea usumbufu wa usafiri wa baharini wananchi wanaosafiri kati ya Unguja, Pemba na Tanzania Bara.
Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar.
Postal Address: 2422 Tel.:0777427449. Fax: 024 2231822

No comments:
Post a Comment