
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linaupongeza uongozi mpya
wa Yanga uliochaguliwa katika uchaguzi mdogo uliofanyika Julai 15 mwaka
huu ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam.
Ushindi waliopata wajumbe wapya sita waliochaguliwa kuingia kwenye
Kamati ya Utendaji unaonesha jinsi ambavyo wanachama wa Yanga
waliohudhuria uchaguzi huo walivyo na imani kwao.
TFF inaahidi kuendeleza ushirikiano wake kwa Kamati ya Utendaji ya
Yanga ambayo hivi sasa ina vinara wapya, na kwamba wana changamoto kubwa
ya kuhakikisha wanaendesha shughuli za klabu hiyo kwa kuzingatia katiba
na kanuni.
Pia tunatoa pongezi kwa Kamati ya Uchaguzi ya Yanga chini ya Jaji
Mkwawa na Kamati ya Uchaguzi ya TFF inayoongozwa na Deogratias Lyatto
kwa kuhakikisha uchaguzi huo unafanyika kwa utulivu na kwa kuzingatia
katiba na kanuni.
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
No comments:
Post a Comment