LONDON, England
KITENDO cha John Terry kushinda kesi yake kimezua mgogoro mpya katika Ligi Kuu England.
Wachezaji weusi wamekasirishwa na kitendo cha Terry kushinda kesi ya kutoa kashfa za kibaguzi dhidi ya beki wa Queens Park Rangers, Anton Ferdinand.
Mahakama ilifuta tuhuma dhidi ya Terry, ambaye alimkashifu mchezaji huyo wakati wa mechi kati ya timu hizo mbili.
Habari zinaeleza kuwa wachezaji weusi wanataka kuunda chama chao kitakachojishughulisha na masuala ya ubaguzi wa rangi kwenye soka.
Pia kuna uwezekano wachezaji weusi wakagoma kusalimiana na Terry wakati wa mechi za Ligi Kuu England.
Rio Ferdinand, ambaye ni kaka wa Anton, alimshutumu vikali beki wa Chelsea, Ashley Cole kwa kumtetea Terry mahakamani.
Rio alidai kuwa Cole alikuwa amefanya kitendo cha usaliti kwa kumtetea Terry.
Chama cha Wanasoka cha England(PFA) kimeonya wachezaji hao kulumbana kwenye intaneti kuhusiana na masuala ya ubaguzi wa rangi.

No comments:
Post a Comment