EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Thursday, July 19, 2012

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar yatangaza siku 3 za maombolezo ya ajali ya MV SKAGIT

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imetangaza siku tatu za maombolezo kuanzia Julai 19 hadi Julai 21 kufuatia maafa ya ajali ya Meli ya Mv. Skagit iliyozama karibu na Kisiwa cha Chumbe Zanzibar.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Ali Mohammed Shein akitangaza maombolezo hayo, alisema bendera zote zitapepea nusu mlingoti na kwamba shughuli za sherehe na burudani zimefutwa kwa muda wa siku tatu za maombolezo.

Dk. Shein alisema shughuli za Serikali zitaendelea kama kawaida. Katika taarifa yake aliyoitoa Ikulu usiku wa kuamkia Julai 19, Rais Dkt. Shein amewahakikishia wananchi na hasa waliopoteza jamaa zao kuwa Serikali itabeba gharama zote za mazishi na pia kugharamia huduma za matibabu kwa majeruhi.

“Nimesikitishwa sana na msiba huu, Katika wakati huu si vema tukaanza kulaumiana jambo la muhimu hivi sasa ni kuokoa maisha ya watu” Alisema Rais Dkt. Shein.

Mbali ya taarifa hiyo, Rais Dkt. Shein aliungana na wananchi, viongozi wa Serikali, vyama vya siasa, Viongozi wa dini katika kutambua maiti zilizofikishwa katika eneo maalum la viwanja vya Maisara Suleiman.

Mbali ya kwenda katika viwanja hivyo, pia alifika katika eneo la bandari ya Zanzibar kufuatilia taarifa za tukio hilo. Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jana lilisitisha shughuli zake kufuatia maafa hayo ambapo wakati wa jioni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Emmanuel Nchimbi alitarajiwa kufanya majumuisho ya bajeti yake.

Baadhi ya Wabunge wakiongozwa na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Shamsi Vuai Nahodha, Mkuu wa Jeshi la Polisi walitembelea majeruhi katika Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja pamoja na eneo la viwanja vya Maisara ambapo maiti hufikishwa kwa ajili ya utambuzi.

Mbali ya Bunge, pia Baraza la Wawakilishi Zanzibar jana lilisitisha kwa muda shughuli zake ili kutoa nafasi kwa Wawakilishi hao wa wananchi kushiriki katika shughuli za uokozi ambapo wengi walifika bandarini kusaidia kazi mbalimbali ikiwemo kuwafariji waliopoteza ndugu zao.

Taarifa kutoka Mamlaka za Serikali zinaeleza kwamba hadi asubuhi hii maiti 30 zilipatikana ambapo 20 kati ya hizo zimetambuliwa na kuchukuwa na jamaa zao huku wananchi wengine wakiendelea na kuzitambua maiti zinazofikishwa katika eneo la Maisara.

Aidha, katika taarifa hiyo, watu 145 wameokolewa wakiwa hai, wengi wao wapo katika hali nzuri wameruhusiwa kuungana na familia zao baada ya kupatiwa matibabu katika Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja Zanzibar.

Meli ya Mv. Skagit ilizama Julai 18,2012 saa 7:50 mchana ikitokea Bandari ya Dar es Salaam kwenda Zanzibar ikiwa imebeba abiria 250 watu wazima, watoto 31 na mabaharia 6.

Kazi ya utafutaji na uokoaji zinaendelea asubuhi hii katika eneo la tukio ilikozama meli hiyo umbali wa maili sita Kusini mwa Kisiwa cha Yasin karibu na Kisiwa cha Chumbe Zanzibar.
Juma Mohammed,
MAELEZO Zanzibar 

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate