Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhandisi Evarist Ndikilo , akihutubia waumini
wa dini ya Kiislam ya Jumuiya ya Ahamadia (hawapo pichani)
SERIKALI
imesema migogoro ya kisiasa na kiitikadi ya kidini, kutokuwepo kwa
mgawanyo sawa wa rasimali za nchi kunaweza kuleta uvunjifu wa amani na
utulivu uliopo nchini.
Pia
imewaonya wanasiasa na viongozi wa dini wanaochanganya siasa na mambo
ya kiroho, kwa kisingizio cha cha dini kuacha kufanya hivyo, kwani
wanasababisha uvunjifu wa amani.
Kauli
hiyo ilitolewa jana na Mkuu wa mkoa wa Mwanza, Mhandisi Evarist
Ndikilo, katika mkutano wa amani uliondaliwa na Jumuiya ya Waislamu ya
Ahamadiya jijini hapa, mkutano ambao ulihudhuriwa na Amiri Sheikh Mkuu
wa Jumuiya hiyo nchini, Tahir Mahamood , pamoja na viogozi mbalimbali wa
madhehebu ya dini ya kiislamu na kikristo jijini .
Ndikilo
alisema, wapo viongozi wa dini wanachanganya siasa na mambo ya kiroho ,
wanapofanya hivyo wanavuruga amani ya nchi yetu na kuingiza jamii
katika machafuko, ambapo aliwataka viongozi hao na wanasiasa kuacha
kuchanganya mambo hayo kwani yatasababisha amani ya nchi yetu
kuvurugika.
“Dini
ni kumcha Mungu, lakini siasa ni kuchukua dola au madaraka ya nchi.Wapo
baadhi ya viongozi wa dini wanachanganya siasa na mambo ya kiroho, hao
wanasababisha uvunjifu wa amani.Siasa tuwachie wanasiasa kwenye majukwaa
yao.Serikali inawaunga mkono kutokana na juhudi zetu za kulinda na
kutunza amani tuliyo nayo,” alisema Ndikilo.
Alidai
kuwa zipo kelele za dini kutaka kuhatarisha amani ya nchi yetu, kwani
jumuiya ya dini nyingine ni kuikumbusha nyingine majukumu yake ya
kuhubiri amani , hili litaepusha dhahama kwa nchi yetu.
Alisema
tabia ya vitisho na kukosa uvumilivu kwa baadhi ya dini kuendesha
mihadhara ya kutukanana dini zingine ni kinyume cha maadili, kwamba dini
zikitumika vibaya zitasababisha umwagaji damu.
Ndikilo
alisema kuwa, serikali inawajibika kuheshimu dini hizo na kutoa uhuru
wa kuabudu kwa kila raia wa nchi hii, hivyo dini ni chombo cha
kuunganisha wanadamu na ikitumika vizuri itakuwa ni mhimili wa amani
duniani kote na si Tanzania pekee.
“
Wote mmekiri hapa kuwa, amani ikitoweka wote tutaathirika,bila amani
hakuna mtu atafanya kazi kwa uhuru,kila mtu atatafuta pa kutokea, hivyo
mchango wenu madhehebu ya dini katika kudumisha amani nchini ni
mkubwa.Mmekuwa mkihubiri amani na upendo kwa kutumia neno lenu ‘mapenzi
kwa wote bila chuki kwa yeyote’ lakini pia msmamo wenu wa kufuata
sheria .Hakuna serikali inataka wananchi wake wasifuate sheria,” alisema
Ndikilo alisema migogoro ya kisiasa na kiitikadi inaweza kuhatarisha amani ya nchi kutokana na mgawanyo usio sawa wa rasilimali za nchi, kwamba ubaguzi wa rangi, kijinsia,ukabila , ukanda na udini unaweza kuvunja amani ya nchi.
Hata
hivyo alisema ni ndoto kufikiri kuwa Usilamu ama Ukristo utatoweka kwa
kupitia mihadhara au kwa kuchoma Makanisa na Misikiti, kwani yalikuwepo
na yartaendelea kuwepo duniani.Kwamba kuvumiliana na kuacha kuzungumza
kwa hisia kutadumisha misingi ya amani ya nchi yetu.
Ndikilo
aliwataka viongozi wote wa dini kusaidiana na serikali katika kupiga
vita rushwa,mauaji ya walemavu wa ngiozi, mauaji ya vikongwe na
mamambukiz ya virusi vya ukimwi kwa kluwa yote hayo hayachagui imani ya
mtu.
Pia
alisema kuwa amani huanza kujengwa katika ngazi ya familia na kuitaka
jamii kukemea wizi (vibaka) uvaaji wa nguo fupi za nusu uchi na kuwalea
watoto katika maadili mema, kwani huo ndio mwanzo wa amani katika ngazi
ya familia.
Alisema watoto kutukana wakubwani malezi mabaya, na baadhi
ya viongozi wa kisiasa kutukana viongozi wa kitaifa kwa kisingizio cha
siasa ni uvunjifu wa amani nchini, ambapo alidai ushoga ambao upo katika
familia lakini unafumbiwa macho nao ni cghanzo cha kuvunjika kwa amani.
“Kila
mmoja ashiriki shughuli za maendeleo akiwa ana amani, waathirika
wakubwa ni watoto na akina mama, lazima tuienzi amani tuliyo nayo kwa
gharama yoyote , kila mmoja akiwajibika katika eneo lake nchi yetu
itakuwa salama na amani,” alisema Ndikilo
Awali
Amiri Sheikh Mkuu wa Jumuiya ya Waislamu wa Ahamadiya, Tahir Mahamood
alisema kuwa alisema Quran inaelekeza kuhusu suala la amani na jinsi ya
kupeleka ujumbe unaohusiana na amani.
Alisema
falsafa ya Uislamu ni amani ni zawadi (tunu) kutoka kwa Mungu,n
kukumbushana na jamii kuwa tunu hiyo (amani) tuitunze,kuipoteza ni
rahisi lakini kuirejesha ni gharama kubwa.
Alidai makundi mengi yanayojihusha na mauaji yakiwemo yale ya kigaidi, yanafanya hivyo kutokana na uelewa mdogo na kinyume na imani ya dini ya Kiislamu kwa vile haifundishi hayo.
“Vipo
vikundi vya kigaidi vinatumia dini kufanya udhalimu.Waisalmu wengi
wanatumiwa kujilipua, Wailsmu walikufa kwa kutetea imani ya dini yao,
lakini si wale wanaojivika mabomu na kujilipua.Kwamba mtizamo huo
umepokelewa na baadhi ya mashaeikh wa dini ya Kiislamu,kinyume na
mafundisho ya mtume,” alisema Amiri Sheikh Mahamood na kuongeza;
“ Mtume
hakuletwa kwa ajili ya kujilipua, au kupambana na watu, alikuja
kuwafikishia ujumbe wa wazi wazi,kwa anayetaka aamini na kutoa huduma
kwa watu lakini si kuwauwa..
Alisema
dini ya kiislamu inashirikiana na dini zingine na misahafu yote ya dini
inafundisha hivyo, na kuwataka Waislamu kutovunja makanisa wala
misikiti kwa kuwa hizo ni nyumba za ibada.
Viongoizi
wa dini mbalimbali za Kiislamu,Kikristo na Kihindu walihudhuria mkutano
huo wa amani, ambao ulifanyika kwenye ukumbi wa Nyerere katika hoteli
ya Gold Crest, hapa.

No comments:
Post a Comment