Jeshi la Polisi mkoani Morogoro, linamshikilia Tausi Kapera (24) mkazi
wa Njia Nne, Ngerengere, kwa tuhuma za kuwanywesha watoto wake sumu ya
panya, pamoja na yeye mwenyewe kwa lengo la kutaka kujiua, baada ya
kutokea ugomvi kati yake na mume wake.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Faustine Shilogile, aliwataja watoto hao kuwa ni Abdulazizi Hamisi (mwenye umri wa mwaka mmoja na miwezi mitatu) na Ramadhani Khamisi (6).
Alisema Tausi alitenda kosa hilo juzi, saa 12 jioni, huko Njia Nne, Ngerengere.
Alisema kabla ya kunywa sumu hiyo, alianza kuwanywesha watoto wake, kisha naye akanywa, chanzo kikiwa ni ugomvi kati yake na mume wake, Khamisi Asan, ambaye ni askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), 121 KJ Sangasanga.
Alisema watoto hao pamoja na mama yao, wamelazwa katika Kituo cha Afya Ngerengere, kwa ajili ya matibabu, huku mwanamke huyo akiwa chini ya ulinzi wa polisi.
Alisema atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma hizo, baada ya kuruhusiwa kutoka hospitali.
via MTANZANIA

No comments:
Post a Comment