Mkurugenzi wa Global Publishers, Eric Shigongo(kati) akizungumza
na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya msanii huyo na kushoto ni
Meneja Mkuu wa Global Publishers, Abdallah Mrisho.
John Dilinga, 'DJ JD', nae akiwaeleza wanahabari jinsi alivyotapeliwa na Chameleone mwaka 2005.
Baadhi ya wanahabari wa vyombo mbalimbali vya habari wakimsikiliza kwa makini Eric Shigongo.
JD akisisitiza jambo (kulia) Juma Mbizo, Mratibu wa Matamasha.
Eric Shigongo (kulia) akisikiliza maswali kutoka kwa waandishi wa habari.
MD wa Global Publishers Ltd, Eric Shigongo, mapema leo ameongea na
media kuhusu madai ya Jose Chameleone kudai paspoti yake, ambaye jana
alikwenda Ubalozi wa Tanzania nchini kwake Uganda kushinikiza
kurejeshewa paspoti yake.
Eric amefunguka kwa kusema kuwa, kampuni yake na msanii huyo
waliingia makubaliano ya kufanya shoo kwenye Tamasha la Usiku wa
Matumaini, liliofanyika Uwanja wa Taifa Julai 7 mwaka huu, ambapo katika
mazungumzo ya awali, msanii huyo aliomba kulipwa dola 5000 na kulipiwa
tiketi 2 za ndege ili kuhudhuria tamasha hilo, masharti ambayo
yalikubaliwa.
Mazungumzo hayo ya awali yalifanyika kati ya Global Publishers na
agenti wa Chameleone ajuliikanae kwa jina la George. Kabla ya kutuma
fedha hizo, kampuni yake ilihitaji kujiridhisha kama ajenti huyo alikuwa
kweli anawasilina na kukubaliana na Chameleone kuhusu shoo ya Dar, ili
kuepuka utapeli.
“Tulipokubaliana nae kupitia ajenti wake, tuliamua kwenda mbele
zaidi ili kujiridhisha, ambapo tuliwasiliana na mwanamuziki Kidumu
ambaye anamfahamu huyo George na kwenda mpaka Kampala kukutana ana kwa
ana na wahusika, kwa niaba yetu”, alisema Shigongo.
Akielezea zaidi, Shigongo alisema kuwa Kidumu alikwenda Kampala na
kukutana na George pamoja na Jose Chameleone, ambaye alikubali kuja
kufanya shoo na kumruhusu Kidumu kusainishana mkataba na ajenti wake na
kumpatia hizo fedha.
“Chameleone alitoa ruhusa kwa ajenti wake kusaini mkataba na kupokea
advace ya dola 3,500 kwa niaba yake kwa madai kuwa yeye asingeweza
kusubiri malipo wakati huo kwa sababu alikuwa anawahi sehemu nyingine.
“Baadae Jose alikuja kugeuka na kudai hakupewa hizo pesa na ajenti
wake, kitu ambacho kilonekana kama mchezo wa kitapeli kati ya Chameleone
na ajenti wake kwetu sisi.
“Kwa kuwa ujio wake Tanzania ulikuwa umeshatangazwa sana, uongozi wa
Global Publishers, ulilazimika kufanya mazungumzo mengine na Chameleone
na kumuomba sana kuja nchini kufanya shoo, ambapo this time akakubali
kwa masharti ya kulipwa dola 8000 na tiketi nne za ndege.
“Ndugu zangu, sikua na jinsi, nililazimika kumkubalia na kumlipa dola
8000, kwa sababu tayari tamasha lilikuwa limeshatangazwa sana,
billboards zimewekwa barabarani na promosheni kubwa ilikuwa inafanyika,”
alisema Shigongo kwa uchungu.
Hivyo mara baada ya kukubaliana, safari hii akalazimika kumtuma
meneja wake kwenda mpaka Kampala na kukutana na Chameleone ana kwa ana
na kumpatia dola 8000 na kusaini mkataba mwingine wa pili.
“Ni dhahairi kabisa alichokifanya Chameleone kilikuwa ni utapeli kwa
kushirikiana na ajenti wake, kwa sababu tunamuamini Kidumu ambaye
tumeshafanya naye kazi mara Kadhaa kwa uaminifu mkubwa. Pia ni
Chameleone ndiye aliyemuidhinisha ajenti wake kuchukua pesa hizo, hivyo
ulikuwa ni mchezo wa pamoja, na hiyo ni tabia ya Chameleone, kwani
ameshawafanyia mapromota wengi kiasi kwamba hivi sasa hakanyagi nchini
Kenya.
“Dola 3,500 siyo fedha nyingi, ningeweza kuzisamehe, lakini nimeamua
kuzidai kwa manufaa ya watu wengine, Watanzania tusikubali kufanywa
wajinga kwa sababu ya upole wetu, tutaendelea kudhauriwa na kufanywa
wajinga mpaka lini,” alihoji Shigongo.
Mwisho Shigongo alitoa wito kwa Watanzania kuungana katika suala
hili, kwani Chameleone ameonesha dharau kubwa kwa Watanzania kwa
kumfuata balozi wetu nchini Uganda na kuondoka ofisi kwake huku akisonya
na kubamiza mlango, akiendelea kuonesha dharau kwa Watanzania wote
wapatao miloni 40!
PICHA: ISSA MNALLY/ GPL
No comments:
Post a Comment