Mgomo
wa walimu wa nchi nzima ni dhahiri kuwa umeiva baada ya msuluhishi
aliyeteuliwa na Tume ya Usuluhishi na Uamuzi kutangaza kuwa ameshindwa
kusuluhisha mgogoro huo kati ya Chama cha Walimu Tanzania (CWT) dhidi ya
serikali.
Rais wa CWT, Gratian Mukoba, alisema jana jijini Dar es Salaam kuwa msuluhishi Cosmas Fimbo Msigwa aliyeteuliwa na tume hiyo ametoa cheti cha kuthibitisha kuwa mgogoro umeshindikana kusuluhishwa kwa mujibu wa sheria.
Mukoba alisema kifungu cha 80-(1) cha Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini ya mwaka 2004, kinaeleza kuwa ikiwa mgogoro wa kimaslahi kama ulivyo wa CWT na serikali unaposhindikana kusuluhisha, chama cha wafanyakazi kinachukua hatua ya kuwajulisha wanachama wake wapige kura kukubali au kukataa kugoma.
“Julai 25, mwaka huu CWT na serikali walifika mbele ya msuluhishi kupewa cheti cha kuonyesha kuwa usuluhishi umeshindikana, kwa maelezo hayo CWT kimewaagiza wanachama wake kuanza kupiga kura tangu juzi ya kukubali kugoma baada ya kupewa cheti hicho,” alisema Mukoba.
Alisema ikiwa walimu wengi watakubali mgomo huo kuliko watakaokuwa wamepinga, Baraza la Taifa la CWT litakutana kwa dharura kutangaza mgomo kwa kuwaeleza wanachama na serikali kuhusu aina ya mgomo ambao utakuwa umeamriwa.
Mukoba alisema baada ya baraza hilo kutoa uamuzi, CWT itatoa notisi ya saa 48 kwa Katibu Mkuu Kiongozi ambaye ni Mkuu wa Utumishi wa Umma kumwarifu tarehe ya kuanza kwa mgomo ili alinde mali zake kama sheria inavyoelekeza.
“Walimu hawana nia mbaya na watoto, lakini ugumu wa maisha na ukaidi wa serikali kutotilia maanani mahitaji ya walimu ndiyo iliyotufikisha hapa,” alisema Mukoba na kuwataka walimu kupiga kura za kukubali mgomo hata nyakati za usiku ili kufikia malengo.
Alisema Julai 20, mwaka huu serikali ilifika mbele ya Msuluhishi ikiwa na hoja tatu, moja ikidai CWT kiwasilishe takwimu za walimu wanaopaswa kulipwa ili ifanye hesabu kuona kama ina uwezo kwa kuwa serikali haijui takwimu za walimu.
Mukoba alisema hoja hiyo ya serikali ilikuwa na nia ya kupotosha ukweli wa madai ya walimu kwa kuwa Julai 10, mwaka huu serikali iliwasilisha taarifa kuwa imeshatumia Sh. trilioni nne kulipa mishahara ya walimu, sasa iweje itake takwimu za idadi ya walimu.
Alisema hoja nyingine ya serikali ilieleza kuwa haijui idadi ya walimu wanaofundisha masomo ya sayansi na walimu wanaofanya kazi kwenye mazingira magumu, hivyo haiwezi kukokotoa hesabu na kuitaka CWT kuwasilisha takwimu hizo.
Aliongeza kuwa hoja hizo zilipingwa na CWT kwa kuwa serikali ndiyo yenye shule za mchepuo wa sayansi na inafahamu walimu wa sayansi ni wangapi nchini kwa kuwa takwimu hizo zilishatolewa na Bunge wakali wa maswali na majibu.

CHANZO:
NIPASHE
No comments:
Post a Comment